Kiongozi mkuu wa DPRK Kim Jong Un asimamia mafunzo ya vikosi vya operesheni maalum: KCNA

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 30, 2026

Picha hii iliyotolewa na Shirika Kuu la Habari la Korea (KCNA) ikimuonyesha Kim Jong Un, katibu mkuu wa Chama cha Wafanyakazi cha Korea (WPK) na Rais wa Masuala ya Nchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK), akisimamia kambi ya mafunzo ya operesheni maalum iliyo chini ya mamlaka ya moja kwa moja ya idara ya Operesheni ya Makao Makuu ya Jeshi la watu la Korea. (KCNA/kupitia Xinhua)

PYONGYANG - Kim Jong Un, kiongozi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) amesimamia mafunzo ya vikosi vya operesheni maalum wakati wa ziara yake kwenye kambi kuu ya mafunzo, Shirika la Habari la Korea KCNA limeripoti jana Jumapili.

Kwenye kambi ya mafunzo ya operesheni maalum iliyo chini ya mamlaka ya moja kwa moja ya Idara ya Operesheni ya Makao Makuu ya Jeshi la Watu la Korea, Kim Jong Un, katibu mkuu wa Chama cha Wafanyakazi cha Korea (WPK) na Rais wa Masuala ya Nchi wa DPRK, ameviagiza vikosi vya jeshi la nchi hiyo kujiandaa kikamilifu kulingana na mwelekeo wa vita vya kisasa, akisisitiza kile alichokiita ukweli usiopingika: "Kadiri jasho linavyoongezeka wakati wa mafunzo ya amani, ndivyo damu inavypungua katika uwanja wa vita," imesema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kiongozi huyo wa DPRK ameweka mpango wa kuvipanga upya vikosi vya operesheni maalum pamoja na hatua za ufuatiliaji.

Imesema kwamba, mafunzo hayo yalilenga kutathmini uwezo wa kimwili na wa kijeshi wa wanajeshi katika vikosi vya operesheni maalum.

Picha hii iliyotolewa na Shirika la Habari la Korea (KCNA) ikimuonyesha Kim Jong Un, katibu mkuu wa WPK na Rais wa Masuala ya Nchi wa DPRK, akisimamia kambi ya mafunzo ya operesheni maalum chini ya mamlaka ya moja kwa moja ya Idara ya Operesheni ya Makao Makuu ya Jeshi la Watu wa Korea nchini DPRK. (KCNA/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha