Lugha Nyingine
Rais Xi ahimiza kuhamasisha jamii nzima katika juhudi za kupanda miti

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akipanda mti kwenye shughuli ya kujitolea kupanda miti katika mji mdogo Baishan wa Eneo la Changping la Beijing, mji mkuu wa China, Machi 30, 2026. (Xinhua/Yan Yan)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ametoa wito wa kuhamasisha jamii nzima kufanya juhudi za kushiriki katika upandaji miti, akisisitiza kwamba mazingira mazuri ya ikolojia yanawanufaisha watu wote na yanahitaji juhudi za pamoja za watu wote.
Rais Xi, ameyasema hayo jana Jumatatu alipokuwa akishiriki kwenye shughuli ya kujitolea kupanda miti mjini Beijing.
Rais Xi na viongozi wengine wa Chama na serikali, wakiwemo Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi, jana asubuhi walifika katika sehemu ya kupanda miti katika Eneo la Changping la Beijing. Rais Xi aliupungia mkono kuwasalimia umati wa watu kisha alichukua koleo kushiriki kwenye shughuli hiyo. Amepanda miche ya aina mbalimbali za miti.
Wakati akipanda miti hiyo, aliwauliza watoto walioshiriki shughuli hiyo kuhusu masomo yao na maisha yao ya kila siku, ushiriki wao kwenye kazi na michezo, na kushiriki kwao katika shughuli za kupanda miti. Amesisitiza umuhimu wa kuweka malengo makubwa wakati wa umri mdogo, kujenga na kuhimiza kupenda masomo, kazi na mazingira ya asili, na kujitahidi kuwa nguzo za jamii.
Rais Xi pia alizungumza na maofisa na watu kwenye sehemu ya kupanda miti. Amesema kwamba nchini China eneo la misitu linaenendelea kupanuka, na maeneo ya jangwa na mchanga yanaendelea kupungua, hali ambayo imeifanya China kuwa nchi yenye eneo kubwa zaidi na ongezeko kubwa na la kasi zaidi la upanuaji wa mazingira ya kijani duniani.
Rais Xi amepongeza “Sheria ya Mazingira ya Ikolojia” iliyopitishwa mwezi wa Machi, akisema sheria hiyo inaimarisha zaidi msingi wa kisheria wa kujenga China Inayopendeza.
"Upandaji miti ni jukumu muhimu katika kujenga China Inayopendeza," Rais Xi amesema, akihimiza kazi husika ziendelee kusukumwa mbele kwa vitendo halisi.
Rais Xi amesema, mwaka huu ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) na maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa harakati za kujitolea kupanda miti kote nchini.
Amesema katika hali mpya ya sasa, juhudi za kuhimiza kazi ya kupanda miti zinapaswa kutilia maanani zaidi kazi yenye sifa bora, kuendeleza viwanda husika, na kutoa manufaa kwa watu.
Rais Xi amesisitiza umuhimu wa kuwezesha njia za kutambua thamani ya bidhaa za kiikolojia, na kufanya mpango wa jumla kwa kusukuma mbele kazi ya kupanda miti mijini na vijijini kote nchini.

Rais wa China Xi Jinping, akipanda mti kwenye shughuli ya kujitolea kupanda miti katika mji mdogo wa Baishan wa Eneo la Changping, Beijing, mji mkuu wa China, Machi 30, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping, akipanda mti kwenye shughuli ya kujitolea kupanda miti katika mji mdogo Baishan wa Eneo la Changping la Beijing, mji mkuu wa China, Machi 30, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

Rais wa China Xi Jinping, akizungumza na umati wa watu katika sehemu ya kufanya shughuli ya kujitolea kupanda miti katika mji mdogo Baishan wa Eneo la Changping la Beijing, mji mkuu wa China, Machi 30, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping, akizungumza na umati wa watu katika shughuli ya kujitolea kupanda miti huko Baishan ya Eneo la Changping la Beijing, mji mkuu wa China, Machi 30, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

Rais wa China Xi Jinping, akizungumza na umati wa katika seheu ya kufanya shughuli ya kujitolea kupanda miti huko Baishan ya Eneo la Changpingla Beijing, mji mkuu wa China, Machi 30, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



