Maonyesho ya Bidhaa za Matumizi kusisitiza mvuto wa kudumu wa soko la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 31, 2026

Watembeleaji wakitazama pikipiki za Ducati kwenye Maonyesho ya 5 ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China (CICPE), Haikou, mji mkuu wa Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Zhou Huimin)

Watembeleaji wakitazama pikipiki za Ducati kwenye Maonyesho ya 5 ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China (CICPE), Haikou, mji mkuu wa Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Zhou Huimin)

BEIJING - Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China (CICPE) yanatarajiwa kusisitiza mvuto wa kudumu wa soko la China, na ushiriki mkubwa wa kimataifa unaonesha imani ya kampuni za kimataifa katika nchi ya China yenye uchumi wa pili duniani kwa ukubwa wake.

Jana Jumatatu naibu waziri wa biashara wa China Sheng Qiuping amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, maonesho hayo yatafanyika katika Mkoa wa Hainan, kusini mwa China kuanzia Aprili 13 hadi 18, ambapo bidhaa za chapa zaidi ya 3,400 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 60 zitaoneshwa kwenye maonesho hayo.

Amesema bidhaa za kimataifa zitakazooneshwa kwenye maonesho hayo zitachukua asilimia 65 ya zile za jumla, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 kuliko mwaka jana.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021, maonyesho hayo yamekuwa jukwaa muhimu kwa kampuni za kimataifa kufahamishwa mwelekeo na mawimbi ya matumizi katika soko kubwa la China, na kampuni zaidi ya 3,800 na bidhaa za chapa zaidi ya 12,000 kutoka nchi na maeneo 92 zilishiriki kwenye maonyesho hayo matano yaliyopita.

Sheng amesema, maonyesho hayo yamekuwa "ngome ya mbele ya daraja" kwa ajili ya ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na mpaka sasa wanunuzi zaidi ya 230,000 wa ndani na nje ya China wameshiriki kwenye maonyesho hayo matano. Waandaaji wamesema kuwa, Canada ikiwa nchi mgeni mheshimiwa wa mwaka huu, italeta kampuni karibu 40 kuonyesha bidhaa za vipodozi, mazao ya kilimo, na chakula cha wanyama vipenzi wa binadamu. Russia na Bulgaria na nyinginezo ni nchi zilizoanzisha mabanda ya kitaifa kwa mara ya kwanza, na ujumbe wa kiserikali wa nchi na maeneo 12, ikiwa ni pamoja na Uswisi, Jamhuri ya Czech na Ireland, pia utashiriki kwenye maonesho hayo.

Waandaaji wamesema, zaidi ya ukumbi mkuu, kutakuwa na eneo la maonesho ya afya huko Boao, ambako kutakuwa na kampuni 120 za kimataifa za dawa na zana na vifaa vya matibabu na afya, na maonyesho ya boti ya Sanya yanatarajiwa kuonesha boti zaidi ya 200, kati ya hizo boti za chapa za kimataifa zikichukua asilimia 70.

Maonyesho hayo ya mwaka huu yana umuhimu mkubwa zaidi kwani hayo ni maonesho ya kwanza tangu Bandari ya Biashara Huria ya Hainan (FTP) ilipozindua kikamilifu uendeshaji maalum wa forodha kote kisiwani mwezi Desemba mwaka jana.

Maonyesho hayo pia yanajiweka kuwa jukwaa la kutangaza mawimbi ya mitindo ya maisha kote duniani, na ni mahali pa kuonesha bidhaa za uvumbuzi mpya zaidi ambapo ni lazima kutembelewa. Bateer, naibu mkuu wa Mkoa wa Hainan amesema, bidhaa mpya zaidi ya 200 zinatarajiwa kutangazwa na kuoneshwa kwa umma kwenye maonyesho hayo ya mwaka huu, bidhaa hizo ambazo zimeongezwa kwa maradufu kuliko mwaka uliopita.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha