Iran yakataa mpango wa kusimamisha mapigano wa Marekani ikiuelezea kuwa ni "uliokithiri sana, usio na uhalisia"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 31, 2026

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, akihudhuria mkutano wa wiki na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, mnamo Machi 30, 2026. (Xinhua/Shadati)

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, akihudhuria mkutano wa wiki na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, mnamo Machi 30, 2026. (Xinhua/Shadati)

TEHRAN - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, amesema kwamba mpango wa kusimamisha mapigano wa hivi karibuni uliopendekezwa na Marekani una madai "yaliyokithiri sana, yasiyo na uhalisia na yenye kukosa mantiki".

Ametoa kauli hiyo jana Jumatatu kwenye mkutano wa wiki na waandishi wa habari mjini Tehran wakati akifafanua juu ya mpango huo wa masharti 15 uliopendekezwa na Marekani uliowasilishwa kwa Iran kupitia wapatanishi ili kumaliza mgogoro huo unaoendelea Mashariki ya Kati.

Baghaei amesema, tofauti na Marekani, "ambayo hubadilisha misimamo yake kila mara, na ambayo maafisa wake hutoa na kuonyesha kauli na tabia zinazokinzana," msimamo wa Iran kuelekea masuala husika umekuwa wazi kabisa tangu mwanzo.

Ameongeza, "Tunajua vizuri sana ni upi mfumokazi wetu tunaoutaka. Kama nilivyosema hapo awali, nyaraka ambazo zimewasilishwa kwetu chini ya vichwa mbalimbali kama vile 'mpango wa masharti 15' zinajumuisha madai yaliyokithiri sana, yasiyo na uhalisia, na yanayokosa mantiki."

Baghaei amesisitiza kwamba "hadi wakati huu, hatujawahi kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani." Amebainisha kuwa tangu raundi ya mwisho ya mazungumzo na Marekani mjini Geneva Februari 26, Iran imepokea ujumbe mbalimbali kupitia wapatanishi fulani, ikiwemo Pakistan, ambao ndani yake ulikuwa na nia na ombi la Marekani kwa ajili ya mazungumzo.

Amesema, Iran haijashiriki katika mikutano iliyoandaliwa na Pakistan na kushirikiwa nanchi jirani.

“Iran itatangaza hitimisho lake kuhusu mpango huo kwa njia inayofaa kwa wakati mwafaka”, Baghaei ameongeza.

Februari 28, Israeli na Marekani zilianzisha mashambulizi ya pamoja dhidi ya Tehran na miji mingine kadhaa ya Iran, yakimuua Kiongozi Mkuu wa wakati huo wa Iran Ali Khamenei, pamoja na makamanda waandamizi wa jeshi na raia. Iran ilijibu kupitia mashambulizi mfululizo ya makombora na droni dhidi ya Israeli na kambi na mali za Marekani katika nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, akizungumza kwenye mkutano wa wiki na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, mnamo Machi 30, 2026. (Xinhua/Shadati)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha