Lugha Nyingine
Faustin-Archange Touadera aapishwa kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
YAOUNDE - Faustin-Archange Touadera ameapishwa rasmi kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati jana Jumatatu kwenye hafla maalum iliyofanyika huko Bangui, mji mkuu wa nchi hiyo.
Rais Touadera amekula kiapo cha kuwa rais kwenye hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Barthelemy Boganda, ambapo wakuu na wanadiplomasia wa nchi mbalimbali wameshiriki kwenye hafla hiyo.
Baada ya kumalizika kwa hafla hiyo, Rais Touadera amewashukuru raia kwa imani yao na kusisitiza kwamba katika muhula wake hili wa kushika madaraka, ataweka mkazo katika kufuatilia hali ya kujiendeleza ya wanawake na vijana, na maendeleo ya nchi.
Pia amesisitiza dhamira yake ya kurejesha amani na utulivu katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita.
Jamhuri ya Afrika ya Kati ilifanya uchaguzi wake wa rais Desemba 28, 2025, na takwimu zilizotolewa na Kamati ya Katiba ya Nchi zimeonesha kuwa, Touadera alipata asilimia 77.9 ya kura zote halali zilizopigwa.
Kuapishwa kwake huko kumeonesha Rais Touadera mwenye umri wa miaka 68 ameanza muhula wake wa miaka saba wa kushika madaraka, ambaye amekuwa rais wa muda wote tangu mwaka 2016. Na muhula hili litakuwa la tatu la kushika madaraka kwake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



