Rais wa China ampongeza Sassou Nguesso kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Kongo

(CRI Online) April 01, 2026

Rais wa China Xi Jinping ametuma ujumbe wa pongezi kwa Denis Sassou Nguesso Jumatatu wiki hii kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Kongo.

Rais Xi amesema, China na Jamhuri ya Kongo zimeendelea kuongeza kuaminiana kisiasa na kuungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi makuu ya kila mmoja, na kutekeleza ushirikiano uliozaa matunda katika sekta mbalimbali.

Amesema kuwa nchi hizo mbili zimeshirikiana kutimiza majukumu yao zikiwa nchi wenyeviti wenza wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, zikibeba jukumu kuu katika kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika na ushirikiano wa nchi za Kusini.

Rais Xi amesema, anaweka umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na yuko tayari kushirikiana na Rais Sassou Nguesso kuboresha zaidi jumuiya ya China na Kongo yenye mustakabali wa pamoja, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha