Rais wa Ghana asema nchi yake iko tayari kushirikiana na China kusukuma mbele zaidi uhusiano wa pande mbili

(CRI Online) April 01, 2026

Rais wa Ghana John Dramani Mahama amesema Jumatatu wiki hii kuwa Ghana iko tayari kushirikiana na China kusukuma mbele zaidi maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.

Rais Mahama ameyasema hayo wakati akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa China nchini Ghana Cong Song katika Ikulu huko Accra.

Amesisitiza tena uhusiano wa kihistoria kati ya Ghana na China, akieleza kuwa mkutano wa mwaka jana kati ya wakuu wa nchi hizo mbili uliofanyika mjini Beijing, China, umezaa matunda tele.

Naye Balozi Cong amesema China iko tayari kutumia vizuri matokeo ya mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na maafikiano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, ili kupata maendeleo zaidi katika uhusiano huo wa ushirikiano wa kimkakati na kuleta manufaa zaidi kwa nchi hizo mbili na watu wao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha