Watu 6 wafariki na wengine 55 wajeruhiwa katika ajali ya basi katikati mwa Tanzania

(CRI Online) April 01, 2026

Polisi na mamlaka husika nchini Tanzania zimethibitisha kuwa basi moja la abiria lilipinduka jana Jumanne mkoani Singida katikati mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 6 na wengine 55 kujeruhiwa.

Ajali hiyo ilitokea kwenye Kijiji cha Mkiwa katika Wilaya ya Ikungi wakati basi hilo lililokuwa likisafiri kutoka Dodoma kwenda Mwanza lilipoingia shimoni katikati ya barabara, na kusababisha tairi ya mbele kupasuka na dereva kushindwa kulidhibiti.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo wa Singida Bw. Amon Kakwale amethibitisha tukio hilo, akisema maafisa waliokuwa katika eneo la tukio waliagizwa kulinda mali za abiria na kutambua watu waliofariki na majeruhi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha