Lugha Nyingine
China na Sudan Kusini zafanya shughuli kuongeza kwa kina uhusiano wa kiutamadani
Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini Jumatano ulifanya shughuli ya siku ya wazi kwa umma kushiriki iliyolenga kuhimiza na kuongeza kwa kina uhusiano wa kiutamaduni kati ya watu wa nchi hizo mbili.
Shughuli hiyo iliyopewa jina la “Ugunduzi wa Panda” ilikutanisha makundi mbalimbali ya kiutamaduni ya wenyeji na maofisa wa serikali. Panda, hazina ya kitaifa ya China na mnyama anayepatikana China pekee, anapendwa sana kote duniani.
Waziri wa utamaduni, makumbusho na urithi wa taifa wa Sudan Kusini Sarah Nyanath Elijah Yong amesema, Sudan Kusini inachangia na China dhamira imara ya kuhifadhi urithi na kuhimiza maendeleo endelevu, na kuhakikisha maendeleo yanapatikana bila kuharibu utamaduni na msingi ya taifa.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini Sudan Kusini Ma Qiang amesema China inasukuma mbele kila wakati ujenzi wa mambo ya kisasa, na kuleta fursa kubwa za maendeleo kwa dunia.
Ameongeza kuwa wakati mwaka huu ni wa maadhimisho ya Mwaka wa Mabadilishano kati ya Watu wa China na Afrika, China itazidi kuimarisha mawasiliano kati ya nchi hizo mbili kwenye nyanja zote, na kuendelea kutoa fursa za masomo na mabadilishano nchini China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



