Daraja la Bonde Kubwa la Mto Huajiang la China lathibitishwa kuwa daraja lililopo juu zaidi duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 30, 2026

Picha iliyopigwa Septemba 28, 2025 ikionyesha mandhari ya Daraja la Bonde Kubwa la Mto Huajiang katika Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Yang Wenbin)

Picha iliyopigwa Septemba 28, 2025 ikionyesha mandhari ya Daraja la Bonde Kubwa la Mto Huajiang katika Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Yang Wenbin)

GUIYANG - Daraja la Bonde Kubwa la Mto Huajiang katika Mkoa wa Guizhou kusini magharibi mwa China limethibtishwa na Rekodi za Dunia za Guinness (GWR) kuwa daraja lililopo juu zaidi duniani, likiwa na kimo kilichothibitishwa cha mita 626.01.

Baada ya upimaji na uthibitishaji wa kurudia mara kadhaa, matokeo hayo yaliyotangazwa Jumanne wiki hii yameonesha rekodi hiyo mpya duniani kwa urefu wa kimo wa daraja hilo, likilipita Daraja la Beipanjiang lenye kimo cha mita 565.4, ambalo linapita Guizhou na mkoa jirani wa Yunnan na lilipewa cheti na GWR mwaka 2018.

"Kimo cha mwisho kilichothibitishwa cha Daraja la Bonde Kubwa la Mto Huajiang ni mita 626.01, ukizidi rekodi ya awali ya dunia ya mita 565.4. Jaribio la kuvunja rekodi limefanikiwa," amesema Luo Qiong, jaji rasmi wa GWR, kwenye hafla ya utoaji wa cheti hicho.

Daraja hilo lililopo katika sehemu ya milimani ya kusini-magharibi mwa China ni daraja lenye fremu ya mihimili ya chuma, na ni mradi muhimu kwenye Barabara Kuu ya Liuzhi-Anlong katika mkoa huo wa Guizhou. Lilizinduliwa Septemba 28, 2025.

Kabla ya kuthibitishwa na Rekodi za Guinness, daraja hilo tayari lilikuwa limevutia ufuatiliaji mkubwa wa sekta ya ujenzi kwa urefu wake wa kati ya nguzo kuu na kimo chake, huku baadhi ya wataalamu wa daraja wakilielezea kuwa ni mradi wa kuweka rekodi katika vipimo vya mlalo na wima.

Sehemu liliko daraja hilo pia imeendelezwa kuwa kivutio cha utalii. Tangu kufunguliwa kwake, lifti zake za kutazamia mandhari, vifaa vya burudani ya kuruka kwenye miinuko mirefu na maonyesho ya mwanga wa taa kwenye pazia za maji vimevutia idadi kubwa ya watembeleaji wakati wa mapumziko ya sikukuu muhimu, ikiwa ni pamoja na Sikukuu ya Taifa ya mwaka jana na Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

Data hizo za kimo zilizotumika kwa ajili ya kuthibitishwa na Rekodi za Guinness zilitolewa kutoka kwa teknolojia za upimaji na uchoraji ramani za China. Zana na vifaa vya uwekaji sahihi wa nafasi vya BeiDou vilivyoundwa nchini China vilitumika kwenye mchakato huo, na viliwahi kusaidia wapanda milima wa China wakati wa kupanda Mlima Qomolangma, kilele cha juu zaidi duniani.

Mwakilishi wa Kundi la Uwekezaji wa Mawasiliano ya Habari la Guizhou, mjenzi wa daraja hilo, amesema kuthibitishwa na Rekodi za Guinness kunawakilisha utambuzi wa kimataifa juu ya uwezo wa uhandisi na upimaji wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha