China yatoa fursa mpya za maendeleo kwa Afrika kupitia sera ya ushuru sifuri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 30, 2026

Mwonyeshaji (wa pili kushoto) akielezea bidhaa za Afrika kwa wageni wakati wa Maonyesho ya nne ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonyesho cha Changsha, mjini Changsha, mkoani Hunan, katikati mwa China, Juni 13, 2025. (Xinhua/Chen Sihan)

Mwonyeshaji (wa pili kushoto) akielezea bidhaa za Afrika kwa wageni wakati wa Maonyesho ya nne ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonyesho cha Changsha, mjini Changsha, mkoani Hunan, katikati mwa China, Juni 13, 2025. (Xinhua/Chen Sihan)

BEIJING - China, kwa sera yake mpya ya ushuru sifuri iliyotangazwa kwa nchi za Afrika pamoja na soko lake kubwa zaidi, itaipatia Afrika fursa mpya za maendeleo na kusaidia nchi za Afrika kukabiliana na msukosuko wa sasa uchumi wa dunia, kwa mujibu wa mamlaka za China.

Wizara ya Biashara ya China imesema katika taarifa yake Jumatano kwamba hatua hiyo mpya ya China itatoa fursa katika nyanja mbalimbali, ikisema kwamba ushuru sifuri utapunguza gharama za bidhaa za Afrika zinazoingia katika soko la China, na hivyo kuzipa nguvu bora za ushindani.

Wizara hiyo imesema kwamba bidhaa za Afrika kama vile kakao kutoka Cote d'Ivoire na Ghana, kahawa na parachichi kutoka Kenya, pamoja na matunda ya jamii ya machungwa na divai kutoka Afrika Kusini, kwa sasa zinakabiliwa na ushuru kati ya asilimia 8 hadi asilimia 30.

Hata hivyo, kuanzia Mei 1 na kuendelea, ilimradi tu bidhaa hizo zinakidhi kanuni husika za mahali zinakotokea na mahitaji ya ukaguzi na karantini, zitafurahia sera ya ushuru sifuri.

"Sera ya ushuru sifuri inaweka mazingira ya kupanua mauzo ya nje ya Afrika kwenda China, huku ikiboresha usambazaji katika soko la China na kuwapa watumiaji chaguo mbalimbali zaidi." Wizara hiyo imesema.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa sera ya ushuru-sifuri itasaidia kuvutia China pamoja na washirika wengine wa biashara kuongeza uwekezaji barani Afrika, kwa kuleta mtaji, teknolojia, vifaa na utaalamu wa usimamizi ili kusindika bidhaa maalumu za Afrika ndani ya nchi husika kabla ya kuzisafirisha kwenda China.

Imesema hatua hiyo itahimiza uundaji na uboreshaji wa minyororo ya viwanda barani Afrika, kuunga mkono ukuaji wa viwanda wa Afrika na kuifanya sekta ya kilimo kuwa ya kisasa. Pia itasaidia kuhimiza ukuaji wenye uwiano na endelevu katika biashara ya kati ya China na Afrika.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, ushuru sifuri pia unatarajiwa kuchochea utofauti wa bidhaa za mauzo ya nje za Afrika, kuongeza thamani ya bidhaa hizo na kuboresha muundo wa mauzo ya nje, jambo ambalo litanufaisha wakulima na kampuni zenye ukubwa mdogo na wa kati, pamoja na kuongeza ajira na kuboresha maisha ya watu.

Wizara hiyo pia inatarajia sera hiyo ya ushuru sifuri itasukuma mbele zaidi ushirikiano kati ya China na Afrika katika maeneo kama biashara ya huduma, biashara ya kidijitali, viwanda vya kijani, na maendeleo endelevu, jambo ambalo litasaidia kuongeza uwezo wa Afrika wa kujitegemea katika maendeleo na kuharakisha mchakato wake wa mambo ya kisasa.

Kamati ya Ushuru wa Forodha ya Baraza la Serikali la China ilitangaza Jumanne wiki hii kwamba kuanzia Mei 1, 2026 hadi Aprili 30, 2028, China itatoza ushuru sifuri, kwa mfumo wa kiwango cha upendeleo cha ushuru, kwa nchi 20 za Afrika ambazo zimeanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China na hazijaainishwa kuwa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo. Hii inafuatia uamuzi wa awali wa nchi hiyo wa kutoza ushuru sifuri kwa asilimia 100 ya bidhaa zote zilizo katika orodha ya ushuru, kuanzia Desemba 1, 2024, kwa nchi 33 za Afrika zilizoko nyuma kimaendeleo ambazo China ina uhusiano wa kidiplomasia nazo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha