Kampuni ya China yaingiza malori ya kutumia umeme ya kubeba mizigo mizito katika sekta ya ujenzi ya Ethiopia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 30, 2026

Picha hii iliyopigwa Aprili 29, 2026 ikionyesha malori yanayotumia umeme ya kubeba mizigo mizito kwenye sehemu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika jimbo la Oromia la Ethiopia. (Xinhua/Geng Xinning)

ADDIS ABABA - Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China (CCCC) imeingiza malori 50 yanayotumia umeme ya kubeba mizigo mizito katika sehemu ya mradi mkubwa wa uwanja wa ndege wa Ethiopia, ili kusaidia kuhimiza usafiri wa kijani na maendeleo katika sekta za usafirishaji na ujenzi nchini Ethiopia.

Kundi hilo la kwanza la malori 50 yaliyoagizwa kutoka China, yalianza rasmi kufanya kazi katika sehemu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, huku mengine 42 yakitarajiwa kuwasili katika wiki zijazo.

Akizungumza kwenye shughuli husika ya malori hayo jana Jumatano, Liu Xiaoguang, konsuli wa Ubalozi wa China nchini Ethiopia, amesema kuingizwa kwa malori hayo katika sekta ya ujenzi ni sehemu ya ahadi ya pamoja ya China na Ethiopia katika kuendeleza usafiri wa kijani. 

"Vitendo vyetu vya pamoja ni hatua halisi za kutekeleza matokeo ya Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika na kulenga kuimarisha hali ya kuhusisha mikakati ya maendeleo ya kijani ya nchi, ili kuunga mkono mpango kabambe wa Ethiopia kuhusu maendeleo ya kijani yanayohimili tabianchi," Liu amesema.

Wei Qiangyu, meneja mkuu wa CCCC Tawi la Ethiopia, amesema kuingizwa kwa malori hayo nchini Ethiopia kunalenga kufikia mafungamano ya maendeleo ya kijani, na uhimizaji wa ulinzi wa mazingira, na pia kutekeleza wajibu wa kijamii katika mzunguko mzima wa maisha ya mradi huo.

Meya wa Mji wa Bishoftu Alemayehu Jara amesema kutumia malori yanayotumia umeme katika mradi huo mkubwa wa uwanja wa ndege wa Ethiopia si kama tu kunaweza kupunguza utoaji wa kaboni na kuboresha ubora wa hewa, bali pia kunaweka mfano kwa mpango wa usafirishaji endelevu katika sekta ya ujenzi.

Serikali ya Ethiopia imekuwa ikihimiza usafiri wa kutumia vyombo vinavyotumia umeme ili uwe sehemu moja ya juhudi za kupunguza gharama za uagizaji mafuta, kupunguza shinikizo kwenye akiba ya fedha za kigeni, na kuhimiza utekelezaji wa malengo ya ulinzi wa mazingira.

Liu Xiaoguang, konsuli wa Ubalozi wa China nchini Ethiopia, akizungumza kwenye hafla ya kuanza kutumia malori yanayotumia umeme katika sehemu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika jimbo la Oromia la Ethiopia, Aprili 29, 2026. (Xinhua/Geng Xining)

Meya wa Mji wa Bishoftu Alemayehu Jara, akizungumza kwenye hafla ya kuanza kutumia malori yanayotumia umeme katika sehemu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika jimbo la Oromia la Ethiopia, Aprili 29, 2026. (Xinhua/Geng Xining)

Wei Qiangyu, meneja mkuu wa CCCC Tawi la Ethiopia akihutubia kwenye hafla ya kuanza kutumiwa kwa malori yanayotumia umeme kwenye sehemu ya ujenzi wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika jimbo la Oromia la Ethiopia, Aprili 29, 2026 (Xinhua/Geng Xinning)

Mfanyakazi akipiga picha na malori yanayotumia umeme ya kubeba mizigo mizito kwenye sehemu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika jimbo la Oromia la Ethiopia, Aprili 29, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

Mfanyakazi akipiga picha na malori yanayotumia umeme ya kubeba mizigo mizito kwenye sehemu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika jimbo la Oromia la Ethiopia, Aprili 29, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

Picha hii iliyopigwa Aprili 29, 2026 ikionyesha malori yanayotumia umeme ya kubeba mizigo mizito kwenye sehemu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika jimbo la Oromia la Ethiopia. (Xinhua/Geng Xinning)

Picha hii iliyopigwa Aprili 29, 2026 ikionyesha malori yanayotumia umeme ya kubeba mizigo mizito kwenye sehemu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika jimbo la Oromia la Ethiopia. (Xinhua/Geng Xinning)

Picha hii iliyopigwa Aprili 29, 2026 ikionyesha malori yanayotumia umeme ya kubeba mizigo mizito kwenye sehemu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika jimbo la Oromia la Ethiopia. (CCCC/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha