Lugha Nyingine
Watu 11 wauawa katika mashambulizi kaskazini magharibi mwa Nigeria
(CRI Online) Mei 05, 2026
Polisi nchini Nigeria wamesema watu 11 wameuawa baada ya kundi la wapiganaji kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika maeneo ya Kankia ya jimbo la Katsina, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi katika jimbo hilo Aliyu Abubakar Sadiq amesema, vikosi vya usalama vilizuia shambulizi moja jumamosi iliyopita, lakini wapiganaji walijikusanya tena jumapili na kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi, na kuongeza kuwa polisi wanaendelea kuwasaka washambuliaji.
Ofisa wa mambo ya ndani na usalama wa jimbo hilo Nasir Mu'azu amesema katika taarifa kuwa, katika operesheni iliyofanyika jumamosi iliyopita dhidi ya washambuliaji hao, vikosi vya usalama viliwaua wapiganaji wengi na kukamata pikipiki 8 pamoja na mifugo iliyotekwa.
(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



