Lugha Nyingine
Rais Xi ataka juhudi zote za uokoaji zifanywe kufuatia mlipuko wa kiwanda cha fataki katikati mwa China uliosababisha vifo na majeruhi kwa watu wengi
(CRI Online) Mei 05, 2026
Rais Xi Jinping wa China ametaka juhudi zote zifanywe kuwatafuta watu ambao hawajulikani walipo na kuwaokoa waliojeruhiwa baada ya mlipuko kutokea Jumatatu alasiri katika kiwanda cha fataki mkoani Hunan, katikati mwa China na kusababisha vifo na majeruhi kwa watu wengi.
Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Kamisheni Kuu ya Jeshi, alitoa agizo hilo akiamuru idara husika kuimarisha ukaguzi na udhibiti wa hatari katika sekta muhimu, kuimarisha usimamizi wa usalama wa umma, na kuongeza juhudi za kulinda maisha na mali za wananchi.
Mlipuko huo uliotokea saa 10 na dakika 40 alasiri kwa saa za Beijing katika kiwanda kimoja cha fataki katika mji wa Liuyang, mkoani Hunan.
(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



