Zimbabwe yajipanga kuimarisha utalii wakati idadi ya watalii kutoka China ikiongezeka

(CRI Online) Mei 06, 2026

Ongezeko la watalii Wachina wanaowasili Zimbabwe linachochea hitaji la wataalamu wanaoongea lugha ya Kichina na kutoa fursa mpya za ajira katika sekta za utalii na huduma, wakati ambapo mapumziko ya siku 5 nchini China ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yakimalizika jana Jumanne.

Mwongoza watalii na mwanzilishi wa kampuni ya ushauri wa Lugha ya Zimgro Tawanda Zimhindo amesema, idadi kubwa ya watalii kutoka China imelazimisha kuboresha ufanisi wa lugha kwa waongoza watalii na wafanyakazi wa hoteli.

Amesema ongezeko hilo la watalii limesababisha kushamiri kwa biashara katika maeneo ya vivutio vya utalii, kutokana na matumizi katika malazi, chakula, na shughuli nyingine za kitalii.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe, nchi hiyo ilipokea watalii 10,366 kutoka China katika robo ya kwanza ya mwaka 2026, ikiwa ni ongezeko kutoka 8,373 katika kipindi kama hicho mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha