Watu 12 wafariki katika ajali mbili za barabarani ndani ya saa 12 katika Jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 06, 2026

Picha hii iliyopigwa Mei 4, 2026 ikionyesha ajali ya barabarani, mjini Kariega, Eastern Cape, Afrika Kusini. (Idara ya Usafiri ya Eastern Cape kupitia Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Mei 4, 2026 ikionyesha ajali ya barabarani, mjini Kariega, Eastern Cape, Afrika Kusini. (Idara ya Usafiri ya Eastern Cape kupitia Xinhua)

CAPE TOWN - Watu 12 wameuawa na wengine 21 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti za barabarani ndani ya saa 12 Jumatatu katika Jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini, mamlaka zimesema.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Idara ya Usafiri ya jimbo hilo, katika tukio la kwanza, watu saba wamefariki kufuatia ajali ya kugongana kati ya teksi ya basi dogo na basi majira ya saa 12 alfajiri Jumatatu mjini Kariega, mji wa viwanda katika jimbo hilo.

Ajali hiyo ilitokea wakati teksi hiyo iliyokuwa imejaa abiria na iliyokuwa ikisafirisha wafanyakazi kutoka KwaNobuhle ilipofanya mzunguko wa ghafla mbele ya basi lililokuwa likija. "Basi hilo kisha liligongana na upande wa abiria wa teksi hiyo," idara hiyo imesema.

"Watu jumla ya 18 walihudumiwa katika eneo la tukio. Wawili wamepata majeraha makubwa, huku wengine wamepata majeraha ya viwango tofauti na kusafirishwa hadi vituo vya afya vilivyo karibu kwa ajili ya matibabu," imeongeza. "Mamlaka zimeanzisha uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo."

Ajali ya pili ilitokea majira ya saa 11:45 jioni siku hiyo hiyo katika barabara kuu ya N10 kati ya Middelburg na Nxuba katika Wilaya ya Chris Hani.

"Watu watano wamepoteza maisha, huku wengine watatu wakipata majeraha baada ya gari moja kupoteza mwelekeo na kupinduka," idara hiyo imesema.

Gari hilo lilikuwa limebeba abiria wanane, akiwemo dereva. Ripoti za awali zinaonyesha kuwa gari hilo lilikuwa limebeba abiria kupita kiasi, na dereva, ambaye ni miongoni mwa waliofariki, inadaiwa alipoteza udhibiti wa gari hilo, na kusababisha ajali hiyo.

Abiria waliojeruhiwa wamesafirishwa hadi hospitali iliyo karibu kwa ajili ya matibabu zaidi, idara hiyo imesema, ikiongeza kuwa chanzo halisi cha ajali hiyo bado kinachunguzwa.

"Tunatoa wito kwa madereva kuweka kipaumbele kwa usalama, kuzingatia viwango vya uwezo wa kubeba abiria na kuepuka tabia ya uzembe. Uwepo wa usimamizi wa utekelezaji wa sheria utaongezeka huku tukifanya kazi ya kuzuia vifo zaidi katika barabara zetu," imesema.

Picha hii iliyopigwa Mei 4, 2026 ikionyesha ajali ya barabarani, mjini Kariega, Eastern Cape, Afrika Kusini. (Idara ya Usafiri ya Eastern Cape kupitia Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Mei 4, 2026 ikionyesha ajali ya barabarani, mjini Kariega, Eastern Cape, Afrika Kusini. (Idara ya Usafiri ya Eastern Cape kupitia Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Mei 4, 2026 ikionyesha ajali ya barabarani, katika wilaya ya Chris Hani, Eastern Cape, Afrika Kusini. (Idara ya Usafiri ya Eastern Cape kupitia Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Mei 4, 2026 ikionyesha ajali ya barabarani, katika wilaya ya Chris Hani, Eastern Cape, Afrika Kusini. (Idara ya Usafiri ya Eastern Cape kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha