China yajibu kuhusu Japan kurusha makombora ya mashambulizi nje ya mipaka yake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 07, 2026

BEIJING - Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema jumatano kwamba makundi ya mrengo wa kulia nchini Japan yanasukuma kuharakishwa kwa urejeshaji wa mfumo wa ujeshi, akiongeza kuwa ujeshi mambo leo wa Japan unaongezeka na kuwa tishio kwa amani na utulivu wa kikanda.

Lin ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari katika alipokuwa akijibu swali kuhusu habari zilizosema kwamba Japan hivi karibuni ilirusha makombora aina ya 88 katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi "Balikatan" kati ya Marekani na Ufilipino, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Japan kurusha makombora ya mashambulizi nje ya mipaka yake tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Lin amesema kuwa Japan iliwahi kuivamia na kuitawala kikoloni Ufilipino na nchi nyingine za Asia Kusini-Mashariki, na hivyo kubeba wajibu mkubwa wa kihistoria. Amesema, wakati dunia inapoadhimisha miaka 80 tangu kufunguliwa kwa Kesi za Jinai za Tokyo, Japan ambayo ilikuwa nchi mvamizi, si tu kwamba imeshindwa kujitafakari kwa kina uhalifu wake wa kihistoria, lakini pia imetuma vikosi vya kijeshi nje ya nchi na kurusha makombora ya mashambulizi kwa kisingizio cha ushirikiano wa kiusalama.

Lin amesema huo ni mfano mwingine wa juhudi za makundi ya mrengo wa kulia nchini Japan za kuharakisha urejeshaji wa mfumo wa ujeshi kwa nchi hiyo. Amesema, makundi hayo yamekuwa yakikiuka mara kwa mara sera ya Japan ya kujilinda pekee na kanuni husika za sheria za kimataifa na za ndani. Amesema baadhi ya sera na hatua zao hizo zimeenda mbali zaidi ya wigo wa kujilinda.

Msemaji huyo amesema, ukosefu mkubwa wa elimu kuhusu historia ya kweli, pamoja na mitazamo potofu kuhusu historia, vikichochewa na mikakati ya kujiimarisha tena kijeshi na maandalizi kwa ajili ya vita, vimesababisha kuibuka kwa ujeshi mamboleo nchini Japan na kuweka amani na utulivu wa kikanda katika tishio.

"Tunaisihi Japan kujitafakari kwa kina historia yake ya uchokozi wa kijeshi, na kuheshimu ahadi zake, na kuchukua tahadhari katika masuala ya kijeshi na usalama," Lin ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha