Ghana yahimiza muunganyiko wa kidijitali ili kuongeza haki ya kujiamulia ya uchumi wa Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 07, 2026

Makamu Rais wa Ghana Jane Naana Opoku-Agyemang (kulia) akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 3i Africa 2026, Accra, Ghana, Mei 6, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Makamu Rais wa Ghana Jane Naana Opoku-Agyemang (kulia) akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 3i Africa 2026, Accra, Ghana, Mei 6, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA - Makamu Rais wa Ghana Jane Naana Opoku-Agyemang ametoa wito wa kuzitaka nchi za Afrika zihimize muunganyiko wa kidijitali ulio wa kuongeza juhudi, na kuufanya kuwa hatua muhimu ya kuelekea hali ya kuwa na haki ya kujiamulia uchumi barani Afrika.

Opoku-Agyemang amesema jana Jumatano kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 3i Africa 2026 kwamba Afrika lazima ijenge hatua imara za kushirikiana kwa kupitia muunganyiko wa kidijitali.

"Hali ya kujiamulia uchumi yenye thamani sasa pia inategemea muunganyiko, haswa muunganyiko wa kidijitali, kwa sababu hapa ndipo thamani inapotengenezwa, kubadilishana na kudhibitiwa," amesema.

Amesema Afrika tayari imeonyesha uwezo wake wa kupiga hatua kubwa kuvuka mifumo ya zamani. "Kutoa malipo kwa simu, utambulisho wa kidijitali, na teknolojia ya mambo ya fedha vimeonyesha kile kinachowezekana."

Opoku-Agyemang amesema kuwa kazi nyingi zaidi za sasa, ni kuhusu kuhama kutoka upigaji hatua wa nchi moja moja hadi bara zima, na ameongeza kuwa muunganyiko wa uchumi wa kidijitali wa Afrika unahitaji uungaji mkono wa malipo, utambulisho, usimamizi na miundombinu.

Makamu huyo wa rais amesema, kuendelea kuendesha miamala ya ndani ya Afrika kupitia mifumo ya kifedha nje ya bara kunaweza kuongeza gharama na kuahirishwa, wakati huohuo kudhoofisha wazo la kuanzisha soko moja la Afrika kwa kupitia majukwaa kama vile Mfumo wa Malipo na Makazi wa Pan Afrika.

"Hii inahitaji uwekezaji katika miundombinu ya intaneti ya kasi ya wingu. Miundombinu ya wingu na mifumo ya kidijitali lazima pia vije na uratibu wa usimamizi na sera," amesema, akisisitiza kwamba uratibu huo ni muhimu kwa kuhakikisha mamlaka ya data na kulinda haki za watumiaji katika mazingira ya kidijitali.

Ametangaza kwamba Ghana itashirikiana na Zambia, Rwanda, na nchi nyingine katika kufanya majaribio ya kuanzisha ushoroba wa biashara ya kidijitali ya bara, ambao utafuatilia zaidi ushirikiano wa utoaji malipo kwa simu, kutambuana kwa utambulisho wa kidijitali, na ankara za kielektroniki.

Watu wakitembelea kituo cha maonyesho ya uvumbuzi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 3i Africa 2026, Accra, Ghana, Mei 6, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Watu wakitembelea kituo cha maonyesho ya uvumbuzi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 3i Africa 2026, Accra, Ghana, Mei 6, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha