Lugha Nyingine
Sera ya Ushuru-Sifuri Yasaidia Bidhaa Bora za Afrika Kukumbatia Soko Kubwa la China

Maofisa wa Forodha ya Uwanja wa Ndege wa Guangzhou Baiyun wakifanya ukaguzi wa maparachichi freshi kutoka Kenya baada ya sera ya ushuru-sifuri kwa nchi 53 zenye uhusiano wa kidiplomasia na China kuanza kutekelezwa, Mei 1, 2026. (Picha kwa hisani ya Forodha ya Uwanja wa Ndege wa Guangzhou Baiyun)
Tufaha freshi kutoka Afrika Kusini, machungwa freshi ya Misri, maparachichi freshi ya Kenya... Wakati wa likizo ya “Mei Mosi” (Siku ya Wafanyakazi Duniani) ya mwaka 2026, ambapo sera ya ushuru-sifuri ya China ilipanuliwa hadi kuhusisha nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia nayo, mfulilizo wa bidhaa bora za Afrika zilianza kuingia katika soko la China kwa bei za ushindani zaidi, hivyo kufungua nafasi kubwa zaidi ya ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Afrika.
Mapema asubuhi ya Mei Mosi, Kampuni ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya Shenzhen Ouheng iliwasilisha nyaraka ya forodha kwa Forodha ya Uwanja wa Ndege wa Baiyun mjini Guangzhou, iliyo chini ya Idara ya Forodha ya Guangzhou kwa ajili ya shehena ya maparachichi freshi ya zaidi ya kilo 6,900 kutoka Kenya. Baada ya kukamilika kwa ukaguzi na uidhinishaji wa papo hapo uliofanywa na maafisa wa forodha, shehena hiyo ilipita forodhani kwa mafanikio na kufika kwenye meza za walaji wa eneo hilo siku hiyo hiyo.
"Maparachichi katika shehena hii yana sifa ya harufu nzuri, freshi kabisa, na kwa kiasi kokwa ndogo; zaidi, kwa sababu yanapatikana karibu mwaka mzima, yanapendwa sana na walaji wa nchini" Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Yuan Chengjie, amewaambia waandishi wa habari.
Ameongeza kuwa hapo awali kiwango cha ushuru kwa maparachichi freshi yaliyosafirishwa kutoka Kenya kuuzwa China kilikuwa asilimia 7, hivyo utekelezaji wa hatua hiyo ya ushuru-sifuri utasaidia kuimarisha ushindani wa bidhaa sokoni na kusaidia kampuni kupunguza gharama za uendeshaji.
Bara la Afrika lenye maliasili tele huzalisha aina mbalimbali za bidhaa na mazao ghafi, kuanzia nanasi za Benin, pilipili kavu za Rwanda, nyama ya kondoo ya Madagascar, hadi sabuni nyeusi ya Ghana, rozimari (rosemary) ya Tunisia, na mbegu za cassia za Nigeria.
Leo hii, China inafungua milango yake kwa Afrika kwa nguvu zaidi. Ufunguaji mlango huo sio pekee kwa nchi zilizo nyuma kimaendeleo, sera hiyo ya ushuru-sifuri sasa imepanuliwa kikamilifu kujumuisha nchi za Afrika zenye uwezo mkubwa wa kiuchumi – kama vile Afrika Kusini, Misri, Nigeria, na Algeria. Hii ina maana kwamba mtiririko unaoharakishwa wa bidhaa bora zaidi za Afrika uko tayari kuingia katika maelfu ya familia nchini China.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Idara Kuu ya Forodha ya China, mwaka 2025, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi 53 za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia ilifikia dola za kimarekani bilioni 348.08, ikiweka rekodi mpya ya kihistoria. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2026, thamani hiyoya biashara ilikuwa dola bilioni 92.16, ikiwa ni ongezeko la asilimia 26.8 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Ili kukabiliana na ongezeko hilo la idadi ya bidhaa, idara ya forodha ya China inaendelea kuboresha hatua saidizi katika nyanja za uhifadhi na uchukuzi, ukaguzi, na karantini.

Maofisa wa Forodha ya Shanghai wakifanya ukaguzi kwa machungwa kutoka Misri, Mei 1, 2026. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



