Wito kwa Washawishi wa Mitandao ya Kijamii wa Afrika Kutumia Diplomasia ya Kidijitali Kuhimiza Ustawi wa Bara

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 09, 2026

Tarehe 8, Mei, 2026, watu wakihudhuria  kwenye Mkutano wa kwanza wa kilele wa Washawishi wa Mitandao ya Kijamii barani Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia. (Shirika la habari la Ethiopian /kupitia Xinhua)

Tarehe 8, Mei, 2026, watu wakihudhuria kwenye Mkutano wa kwanza wa kilele wa Washawishi wa Mitandao ya Kijamii barani Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia. (Shirika la habari la Ethiopian /kupitia Xinhua)

Mkutano wa kwanza wa kilele wa Washawishi wa Mitandao ya Kijamii barani Afrika ulifunguliwa Ijumaa huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, mkutano huo unalenga kutumia diplomasia ya kidijitali kusimulia hadithi halisi za Afrika kwa dunia.

Mkutano huu wenye kaulimbiu ya "Nguvu za Ushawishi Zahimiza Maendeleo ya Afrika," uliwakutanisha watungaji wa maudhui ya hadithi na wataalamu wa mikakati ya uenezi kutoka zaidi ya nchi 30 za Afrika.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Habari la Ethiopia, Seife Deribe, alisema kwenye shughuli hii kuwa, washawishi wa mitandao ya kijamii barani Afrika wanapaswa kufanya kazi kubwa zaidi katika kubadilisha mitazamo ya watu duniani juu ya Afrika, kwani habari potofu na dhana potofu zilizopitwa na wakati bado zinaendelea kupotosha taswira ya bara hili.

Deribe aliwahimiza washiriki wa mkutano kupinga masimulizi potofu juu ya Afrika na kueneza simulizi za kweli zinazoonesha maendeleo, utamaduni, na uwezo wa bara la Afrika.

Mwana-YouTube wa Ghana na mtungaji wa maudhui ya hadithi za Pan Afrika Bw. Wode Maya, alielezea maoni kama hayo, akiwataka Waafrika kushikilia kueleza hadithi zao wenyewe. "Kama ukitaka kuvunja kumbukumbu zilizokaririwa, basi usisubiri wengine wakusimulie hadithi yako. Lazima uanze kusimulia hadithi za kweli," alisema Maya.

Takwimu zilizotolewa katika mkutano huo zimeonesha kuwa, Afrika inapata hasara za dola bilioni 4.2 kila mwaka kutokana na mitazamo potovu na masimulizi yaliyotungwa na watu wasio Waafrika.

Mkutano huu wa kwanza wa kilele wa Washawishi wa Mitandao ya Kijamii barani Afrika unalenga kuhimiza ushirikiano, kunufaika pamoja na ujuzi, na kuanzisha shughuli za kidijitali kwa kupitia hadithi zao kuwagusa watazamaji zaidi ya milioni 400 duniani kote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha