Lugha Nyingine
Tanzania na Zambia zakubaliana kupunguza vizuizi vya kibiashara
Tanzania na Zambia zimekubaliana kuchukua hatua zaidi kuondoa vizuizi vya kibiashara ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi wa pande mbili, biashara na uwekezaji.
Makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano wa mawaziri wa Kamati ya pamoja ya Biashara uliofanyika Tunduma kwenye mpaka kati ya Tanzania na Zambia, ambako mawaziri na maofisa waandamizi kutoka nchi mbili walikutana kupitia utekelezaji wa maafikiano ya awali na kujadili masuala mapya yanayohusiana na biashara.
Akizungumza katika mkutano huo, naibu waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Bw. Dennis Londo, amesema changamoto karibu 20 za kibiashara zinazoathiri pande zote mbili zimejadiliwa, ambapo saba kati yao zimetatuliwa kwa mafanikio.
Kwa mujibu wa Bw. Londo, masuala yaliyotatuliwa ni pamoja na uratibu wa vigezo wa vipimo vya mafuta kupitia makubaliano ya utambuzi wa pande mbili kati ya mamlaka husika, kuondoa marufuku wa usafiri wa usiku nchini Zambia ili kuruhusu usafirishaji wa mizigo wa masaa 24, uboreshaji wa nyaraka za mizigo kupitia utoaji wa kipindi cha kwanza cha mfumo wa mabadilishano wa taarifa za forodha na kuanza kwa kipindi cha pili cha ujumuishaji wa mifumo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



