Mazungumzo ya vijana wa China na Afrika yafanyika nchini Afrika Kusini

(CRI Online) Mei 09, 2026

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Mazungumzo kati ya vijana wa China na Afrika yamefanyika Alhamis katika mji wa Pretoria, Afrika Kusini, na kukutanisha wawakilishi wa vijana waliobadilishana maoni kuhusu uhusiano wa pande mbili, ushirikiano wa Kusini na Kusini, maendeleo ya vijana na ushirikiano wa pande nyingi.

Chini ya kaulimbiu "Ushirikiano wa Kusini na Kusini katika Dunia ya Pande Nyingi," washiriki walisema ushiriki wa vijana una umuhimu mkubwa katika kuunda ushirikiano duniani.

Rais wa Shirikisho la Vijana wa Afrika Kusini katika Masuala ya Kimataifa (SAYAGA) Lungile Magagula amesema, mazungumzo hayo yanaakisi ahadi ya pamoja ya kuimarisha ushirikiano, kuelewana, na mawasiliano ya watu na watu kati ya Afrika Kusini, China, na Dunia ya Kusini.

Mwakilishi wa Ubalozi wa China nchini Afrika Kusini Li Ao amesema, mwaka huu ni Mwaka wa Mawasiliano ya Watu kati ya China na Afrika, akisema karibu miradi 600 itaendeleza zaidi uungaji mkono wa maendeleo na mawasiliano ya vijana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha