Marais Xi na Trump kujadili uhusiano wa pande mbili, amani na maendeleo duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 12, 2026

BEIJING - Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Guo Jiakun amesema Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Marekani Donald Trump watabadilishana maoni kwa kina juu ya masuala makubwa yanayohusu uhusiano kati ya China na Marekani na amani na maendeleo duniani.

Guo ameyasema hayo jana Jumatatu kwenye mkutano na waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu ziara ijayo ya kiserikali ya Rais Trump nchini China, iliyopangwa kuanzia Mei 13 hadi 15, ambayo itakuwa ziara ya kwanza ya Rais wa Marekani nchini China katika miaka tisa iliyopita.

Marais Xi na Trump walikutana mara ya mwisho Oktoba 2025 mjini Busan, Korea Kusini. Guo amesema, diplomasia ya wakuu wa nchi inafanya kazi ya uelekezaji wa kimkakati isiyo na mbadala katika uhusiano kati ya China na Marekani.

Guo amesema, China inapenda kushirikiana na Marekani katika kufuata moyo wa usawa, kuheshimiana, na kupanua ushirikiano wa kunufaishana, kusimamia na kudhibiti migongano kwa kufaa, na kuingiza utulivu na uhakika zaidi kwenye dunia yenye misukosuko na mabadiliko.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha