Lugha Nyingine
Marais Xi na Trump watembelea Bustani ya Tiantan

Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Marekani Donald Trump wakipiga picha mbele ya Ukumbi wa Kuombea Mavuno Mazuri wakati walipotembelea Bustani ya Tiantan mjini Beijing, Mei 14, 2026. (Xinhua/Shen Hong)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Marekani Donald Trump walitembelea Bustani ya Tiantan jana Alhamisi mjini Beijing ambapo Xi alimpokea Trump nje ya Ukumbi wa Kuombea Mavuno Mazuri, na viongozi hao wawili walipiga picha mbele ya Ukumbi huo na kufanya matembezi.
Katika matembezi hayo, Xi alimwelezea Trump kwamba katika zama za kale, matambiko makubwa ya taifa yalikuwa yamefanyika kwenye Bustani ya Tiantan, ambapo watawala wa China wa wakati huo waliweza kuombea miungu mbinguni kuleta ustawi wa taifa, mapatano ya jamii, na hali nzuri ya hewa ili watu kupata mavuno mazuri.
"Hayo yameonesha wazo la jadi la China kwamba watu ni msingi wa nchi, na msingi huo utakapokuwa ni imara ndipo taifa litakapokuwa na utulivu," Rais Xi amesema.
Amesema Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimerithi na kuenzi wazo hilo linalokita mizizi kwenye ustaarabu wa taifa la China la kutoa kipaumbele kwa umma.
"Kwa kushikilia nia yake ya kimsingi ya kuwahudumia watu kwa moyo wote, Chama kimepata uungaji mkono wa kithabiti kutoka kwa watu wa China, " ameongeza.
Kwa upande wake, Rais Trump amesema amevutiwa na Bustani ya Tiantan yenye historia ya miaka zaidi ya 600. Amesema Marekani na China zote ni nchi kubwa, na watu wote wa nchi hizo mbili ni wenye hekima na wa utukufu.
Ameongeza kuwa nchi hizo mbili zinapaswa kuzidisha maelewano na kuongeza urafiki kati ya watu wao.

Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Marekani Donald Trump wakipiga picha mbele ya Ukumbi waKuombea Mavuno Mazuri wakati walipotembelea Bustani ya Tiantan mjini Beijing, Mei 14, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Marekani Donald Trump wakitembelea Bustani ya Tiantan mjini Beijing, Mei 14, 2026. (Xinhua/Liu Bin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



