Lugha Nyingine
Wanaharakati wa wanyama watoa onyo kuhusu mauzo ya wanyama hai watambaao kutoka Kenya
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya jana Alhamisi mauzo ya nje ya wanyama hai jamii ya reptilia yameongezeka mara kumi kati ya mwaka 2013 na 2023, yakitishia uwiano wa mfumo wa kiikolojia na afya ya umma.
Ripoti hiyo iliyotolewa na Shirika la Ulinzi wa Wanyama Duniani (WAP), inasema kuwa Kenya imeuza nje wanyama hai zaidi ya 870,000 wanaokamatwa na kufungwa katika vizuizi, ambao wameorodheshwa chini ya Mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Spishi za Wanyamapori na Mimea zilizo Hatarini Kutoweka katika muongo uliopita, karibu nusu yao wakiwa ni wanyama jamii ya reptilia.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa mauzo ya nje kwa mwaka ya wanyama hao kwenye masoko ya kimataifa yameongezeka kutoka 8,551 katika mwaka 2013 hadi 86,330 katika mwaka 2023, yakihatarisha maisha ya spishi hizo na kuenea kwa vimelea vya magonjwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



