Xi Jinping aandaa dhifa ya kumkaribisha Trump

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 15, 2026

Rais wa China Xi Jinping akihutubia dhifa kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mei 14, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping akihutubia dhifa kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mei 14, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya dhifa kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump katika ziara yake ya kiserikali nchini China.

Akihutubia dhifa hiyo iliyofanyika jana Alhamisi, Rais Xi amesema uhusiano kati ya China na Marekani ni uhusiano muhimu zaidi wa pande mbili katika dunia ya hivi sasa.

"Lazima tuufanye uhusiano huo uendelee vizuri, na tusiuharibu kamwe," Rais Xi amesema, akiongeza kuwa nchi mbili China na Marekani zinaweza kunufaika kutoka kwenye ushirikiano na zinaweza kupata hasara katika mapambano.

"Nchi zetu mbili zinapaswa kuwa washirika, na hazipaswi kuwa mahasimu," ameongeza.

Rais Xi pia amesema kwamba pande hizo mbili zimekubaliana kuanzisha uhusiano wa kiujenzi wenye utulivu wa kimkakati kati ya China na Marekani ili kuhimiza maendeleo tulivu ya hatua madhubuti, mazuri, na endelevu ya uhusiano kati ya China na Marekani, na kuleta amani, ustawi na maendeleo zaidi kwa dunia.

"Tukikumbuka mchakato wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani, iwe tunaweza kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani, na kuwa na ushirikiano wa kunufaishana au la ni umuhimu wa kuamua uhusiano huo unaweza kusukumwa mbele kwa hatua madhubuti au la," Rais Xi amesema.

Akidhihirisha kuwa uhusiano kati ya China na Marekani unahusiana na ustawi wa watu zaidi ya bilioni 1.7 wa nchi zote mbili na unaweza kuleta athiri kwa maslahi ya watu zaidi ya bilioni 8 duniani, pande zote mbili zinapaswa kubeba wajibu huo wa kihistoria na kuhimiza meli kubwa hiyo ya uhusiano wa China na Marekani kwenda mbele kwa kasi tulivu na katika mwelekeo sahihi.

Katika hotuba yake kwenye dhifa hiyo, Rais Trump amesema pande hizo mbili zimekuwa na mazungumzo ya kuhimiza juhudi na ya kiujenzi.

Rais Trump akisema kuwa uhusiano kati ya Marekani na China ni uhusiano muhimu zaidi wa pande mbili duniani, na nchi hizo mbili zinapaswa kuimarisha ushirikiano ili kujenga siku nzuri za baadaye za dunia.

Rais wa China Xi Jinping akihutubia dhifa kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing,  Mei 14, 2026. (Xinhua/Liu Weibing)

Rais wa China Xi Jinping akihutubia dhifa kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mei 14, 2026. (Xinhua/Liu Weibing)

Rais wa China Xi Jinping akiandaa dhifa kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump katika ziara yake ya kiserikali nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing,   Mei 14, 2026. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping akiandaa dhifa kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump katika ziara yake ya kiserikali nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mei 14, 2026. (Xinhua/Yan Yan)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha