Kundi lenye silaha mashariki mwa DRC latangaza usimamishaji vita wa upande mmoja

(CRI Online) Mei 15, 2026

Kundi lenye silaha la CRP ambalo linafanya shughuli zake kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limetangaza kuwa litatekeleza usimamishaji vita wa upande mmoja kabla ya kile ambacho limekieleza kuwa ni mazungumzo ya awali na serikali ya DRC chini ya upatanishi wa Uganda.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana Alhamisi na kusainiwa na kiongozi wake Thomas Lubanga Dyilo, Kundi hilo la CRP limesema usimamishaji vita huo utaanza kutekelezwa saa sita usiku Alhamisi, ili “kutoa fursa nzuri ya mafanikio” kwa ajili ya mazungumzo ya awali kati ya kundi hilo na serikali huko Kinshasa.

Kundi hilo pia limehimiza upande mwingine kujizuia kufanya “uchokozi wowote” ambao unaweza kusababisha kupamba moto zaidi kwa vita katika Jimbo la Ituri, likisema jimbo hilo halihitaji vurugu zaidi.

Hakukuwa na jibu lolote la mara moja la hadharani kutoka kwa Serikali ya DRC.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha