Mpaka wa Rwanda na DRC wafungwa kwa hofu ya mlipuko wa Ebola

(CRI Online) Mei 18, 2026

Mipaka inayounganisha Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Wilaya ya Rubavu imefungwa jana Jumapili kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DRC.

Meya wa Wilaya ya Rubavu katika Mkoa wa Magharibi wa Rwanda, Prosper Mulindwa amesema kwamba kufungwa kwa mipaka hiyo; ule unaounganisha Goma na mpaka wa Rubavu-Gisenyi kutaendelea kwa muda usiojulikana kama sehemu ya hatua zinazolenga kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo hatari.

Amewasihi wakazi kuendelea kuwa na subira na kutoa ushirikiano, akisisitiza kwamba uamuzi huo umechukuliwa ili kulinda afya ya umma na jamii kutokana na uwezekano wa maambukizi.

Amesema, licha ya kufungwa kwa muda kwa mipaka hiyo, mamlaka za afya zinaendelea kuchunguza Wanyarwanda wanaovuka kutoka DRC, vilevile raia wa DRC wanaorejea nyumbani, ambao bado wanaruhusiwa kutumia vituo vya mpakani chini ya taratibu kali za ufuatiliaji wa afya.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha