Lugha Nyingine
Marais Xi na Putin watuma barua za pongezi kwa Maonyesho ya 10 ya China na Russia
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Russia Vladimir Putin kila mmoja alituma barua za pongezi jana Jumapili kwa Maonyesho ya 10 ya China na Russia, ambayo yamefunguliwa huko Harbin, mji mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China.
Rais Xi amesema kuwa mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Russia, na pia ni maadhimisho ya miaka 25 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Ujirani Mwema na Ushirikiano kati ya China na Russia, Rais Xi amesema ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali umeendelezwa kwa kina na kuimarishwa, na kufikia matokeo yenye matunda kutokana na juhudi za pamoja za nchi hizo mbili.
Katika barua yake hiyo Rais Xi ameeleza matumaini kwamba maonyesho hayo yatakuwa fursa kwa sekta mbalimbali za nchi hizo mbili kutumia hali ya ukaribu wao wa kijiografia na nguvu bora zinazosaidiana, kuendeleza kwa kina ushirikiano wa kufuata hali halisi kwa pande zote, kuhimiza zaidi maendeleo ya uchumi na jamii , na kuongeza siku hadi siku ustawi wa watu wao, na kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo tulivu na ya muda mrefu ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Russia katika zama mpya.
Katika barua yake, Rais Putin amesema maonyesho hayo yameendelezwa kuwa shughuli kubwa zaidi ya maonyesho kati ya nchi hizo mbili, yakitoa jukwaa la kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na ya kina kati ya pande hizo mbili.
Putin ameeleza imani yake kwamba maonyesho hayo yatapata matokeo ya kuhimiza juhudi, kupanga matarajio mapya ya ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili, na kuleta manufaa kwa watu wao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



