China yapongeza hatua ya Ushelisheli kuzuia kibali cha kuingia kwa ndege iliyokuwa imembeba Lai Ching-te

(CRI Online) Mei 19, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema kuwa China inaipongeza Ushelisheli, pamoja na serikali za nchi nyingi rafiki, kwa kuzuia kisheria na waziwazi kibali cha kuingia kwa ndege iliyokuwa imembeba mwakilishi kinara wa vikundi vya kutaka “Taiwan ijitenge” Lai Ching-te.

Wang ameyasema hayo wakati akizungumza na mwezake wa Ushelisheli Barry Faure jana Jumatatu mjini Beijing.

“Inaaminika kwamba nchi zaidi na zaidi, kama Shelisheli, zitasimama upande sahihi wa haki na historia ya kimataifa,” Wang amesema.

Huku akibainisha kuwa mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ushelisheli, Wang amesema China iko tayari kuhimiza ushirikiano wa pande mbili katika uchumi wa kidijitali, wa baharini, wa visiwani, wa kijani na nyanja nyingine ili kusukuma mbele uhusiano wa pande mbili hadi ngazi ya juu zaidi.

Amesema China iko tayari kuchukua utekelezaji kamilifu wa sera ya ushuru-sifuri kwa mataifa yote 53 ya Afrika yenye uhusiano wa kidiplomasia nayo kama njia ya kutoa fursa zaidi za maendeleo kwa nchi za Afrika.

Kwa upande wake, Faure amesisitiza kwamba Ushelisheli inaweka dhamira tena kwa ahadi yake ya kufuata sera ya kuwepo kwa China moja, ambayo haitayumbayumba katika siku zijazo.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha