Msemaji wa China: Ziara ya Putin nchini China inatarajiwa kusukuma mbele zaidi uhusiano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2026

BEIJING – Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China alisema, Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Russia Vladimir Putin watabadilishana maoni juu ya uhusiano wa pande mbili, ushirikiano katika sekta mbalimbali, pamoja na masuala ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa pamoja katika wakati wa ziara ya Putin nchini China.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari wa jana tarehe 18, msemaji huyo amesema Putin atafanya ziara ya kiserikali nchini China kuanzia tarehe 19 hadi 20 Mei kutokana na mwaliko wa Xi Jinping, na hii ni ziara ya 25 ya Rais Putin nchini China.

"Pande hizo mbili zitachukua ziara hii kuwa fursa ya kuendelea kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia hadi kwenye kiwango cha juu zaidi, na kuingiza utulivu zaidi na juhudi kubwa zaidi duniani," msemaji huyo amesema.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha