Wizara ya mambo ya nje ya China yatoa nishani kwa mabalozi wazuri wa nchi mbalimbali nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2026

Wang Yi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China, akishiriki na kutoa hotuba kwenye hafla ya mara ya kwanza ya kutoa nishani kwa Mabalozi wazuri wa nchi mbalimbali nchini China iliyofanyika Beijing, mji mkuu wa China, Mei 18, 2026. (Xinhua/Dai Tianfang)

BEIJING - Wizara ya mambo ya nje ya China imefanya hafla ya mara ya kwanza ya kutoa Nishani kwa mabalozi wazuri wa nchi mbalimbali nchini China iliyofanyika Beijing jana Jumatatu, ili kuwasifu mabalozi hao ambao wametoa mchango muhimu kwa ajili ya kuhimiza uhusiano wa kirafiki kati ya China na nchi nyingine.

Wang Yi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China, alitoa nishani hizo kwa mabalozi wanane au wawakilishi wao.

Waliopewa nishani hizo ni pamoja na mabalozi wa zamani nchini China kutoka Russia, Cambodia, Chad, Uruguay, pamoja na mabalozi wa Pakistan, Kazakhstan, Saudi Arabia na Colombia walioko kazini sasa nchini China.

"Mabalozi ni madaraja ya mawasiliano ya kirafiki kati ya nchi na nchi. Mabalozi wote waliopewa nishani ni marafiki zetu wazuri wanaojua hali ya kina ya China," Wang amesema wakati alipowapongeza mabalozi waliopewa nishani.

Amesema mabalozi hao ni wajenzi wa uhusiano wa pande mbilimbili, ni watangulizi wa kuijua China, ni waongoza njia ya kuhimiza mawasiliano kati ya watu na watu, na ni watu wachangiaji katika ushirikiano wa kunufaishana.

Ameelezea matumaini yake kwamba mabalozi hao wataendelea kutoa mchango kwa ajili ya uhusiano wa kirafiki kati ya China na nchi nyingine.

Mabalozi hao waliopewa nishani wameushukuru upande wa China kwa kutoa nishani hiyo, wakisema kwamba si tu ni utambuzi wa kazi yao bali pia ni uthibitisho wa uhusiano wa ngazi ya juu wa pande mbilimbili.

Wamesema watathamini heshima hiyo na kuendelea kujitolea katika kuzidisha urafiki na China, kupanua ushirikiano wa kunufaishana, kuongeza mawasiliano kati ya watu na watu, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kutimiza matarajio mapana zaidi kwa uhusiano wa pande mbilimbili.

Watu takriban 300, wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali nchini China na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yaliyoko China, pamoja na wajumbe wa China walishiriki kwenye hafla hiyo.

Wang Yi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China (katikati), akishiriki na kutoa hotuba kwenye hafla ya mara ya kwanza ya kutoa nishani kwa mabalozi wazuri wa nchi mbalimbali nchini China iliyofnayika Beijing, mji mkuu wa China, Mei 18, 2026. (Xinhua/Dai Tianfang)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha