Mlinzi alinda misitu ya mikoko kusini mashariki mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2026

Liu Xinmin (kulia) na mfanyakazi wa ofisi ya maliasili ya mji wakikagua ukuaji wa mikoko mipya iliyopandwa kwenye Mto Luoyang katika Mji wa Quanzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Mei 15, 2026. (Xinhua/Jiang Kehong)

Kwenye mlango wa Mto Luoyang katika Mji wa Quanzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China misitu mikubwa ya mikoko inastawi kando ya Daraja la Luoyang, ambalo ni mabaki muhimu ya kale ya kitamaduni la uhifadhi wa kitaifa nchini China. Katikati ya mikoko hiyo, Liu Xinmin mwenye umri wa miaka 76 kila siku anaendesha mashua kufanya doria kwenye maji .

Liu amekuwa akilinda mikoko hiyo tangu mwaka 2002, wakati mji huo ulipoanzisha miradi mikubwa ya urejeshaji wa mifumo ikolojia ya mikoko ili kuboresha ubora wa maji na kulinda mazingira ya asili ya eneo hilo.

Mifumo ikolojia ya mikoko hiyo, iliyoko katika eneo la pwani lenye wastani wa mawimbi ya kiwango cha juu zaidi na cha chini zaidi linalounganisha ardhi na bahari katika maeneo yanayoweza kufunikwa na maji ya bahari kila baada ya muda, ni eneo la mifumo ikolojia ya kipekee ya pwani yenye thamani kubwa ya kiikolojia, kijamii na kiuchumi. Inaonesha umuhimu wake mkubwa katika kuunga mkono shughuli za uvuvi kwenye bahari ya karibu , kusafisha mazingira, na kuongeza ufyonzaji wa kaboni.

Hivi leo, mto huo unasifika kwa maji safi na viumbe hai vingi vya majini, na umekuwa eneo la vivutio kwa wakazi na watalii. "Hivi sasa maisha yetu yameboreshwa zaidi," Liu amesema.

Picha ikimuonyesha Liu Xinmin akifanya doria kwenye Mto Luoyang katika Mji wa Quanzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Mei 15, 2026. (Xinhua/Jiang Kehong)

Picha ikimuonyesha Liu Xinmin akifanya doria kwenye Mto Luoyang katika Mji wa Quanzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Mei 15, 2026. (Xinhua/Jiang Kehong)

Picha ikionyesha misitu ya mikoko na Daraja la Luoyang katika Mji wa Quanzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Mei 15, 2026. (Xinhua/Jiang Kehong)

Picha ikionyesha misitu ya mikoko na Daraja la Luoyang katika Mji wa Quanzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Mei 15, 2026. (Xinhua/Jiang Kehong)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha