Televisheni ya taifa ya Israel yasema Marekani na Israel zimekamilisha maandalizi ya uwezekano wa mashambulizi dhidi ya Iran

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2026

JERUSALEM - Marekani na Israel zimekamilisha maandalizi ya pamoja kwa ajili ya uwezekano wa kuanza tena kwa operesheni za kijeshi dhidi ya Iran, Kan TV ya Israel imeripoti jana Jumanne, ikimnukuu maneno aliyosema ofisa wa usalama wa Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump anatazamiwa kufanya uamuzi "punde," ofisa huyo amesema. Mapema siku hiyo ya Jumanne, Trump alisema huenda Marekani inahitaji kuishambulia Iran tena, kabla ya hapo alisema kuwa ameahirisha shambulio lililokuwa limepangwa.

"Marekani na Israel zinaratibu kwa pamoja kikamilifu. Hakuna upande utakaoshangazwa kama uamuzi utafanywa wa kuanza tena vita," ofisa huyo aliyenukuliwa amesema.

Habari zimesema, jeshi la Israel pia linaimarisha hatua za kujilinda kutokana na wasiwasi wake kwamba maneno aliyosema Trump na majadiliano ya watu hadharani yanayoendelea kila siku kuhusu mapigano hayo mapya huenda vinaweza kuichochea Iran kuanzisha shambulio la kwanza dhidi yao.

Serikali ya Israel bado haijatoa maoni yake juu ya uwezekano huo wa hatua mpya za kijeshi dhidi ya Iran.

Licha ya ripoti hizo, makao makuu ya amrijeshi ya Jeshi la Israeli imesema kwamba, "kufuatia tathmini ya hali ya mambo," miongozo yake ya ulinzi haitabadilika na itaendelea kuwa katika utayari wa kazi angalau hadi Jumamosi usiku.

Pia siku hiyo ya Jumanne, Jeshi la Israeli lilisema meja mmoja amefariki dunia katika mapigano na wapiganaji wa Hezbollah kusini mwa Lebanon.

Ofisa huyo ametambuliwa kwa jina la Itamar Sapir, mwenye umri wa miaka 27, ambaye alikuwa naibu kamanda msaidizi wa jeshi la akiba kutoka makazi ya Ariel ya Ukingo wa Magharibi. Jeshi hilo limesema "amefariki dunia vitani kusini mwa Lebanon."

Naye ni mwanajeshi wa 21 wa Israeli aliyekufa kwenye medani nchini Lebanon tangu mapigano yalipoanza tena mwanzoni mwa mwezi Machi.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha