Putin awasili Beijing kwa ziara ya kiserikali nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2026

Rais wa Russia Vladimir Putin akiwasili Beijing Mei 19, 2026, kwa ziara ya kiserikali nchini China. (Xinhua/Gao Jie)

Rais wa Russia Vladimir Putin akiwasili Beijing Mei 19, 2026, kwa ziara ya kiserikali nchini China. (Xinhua/Gao Jie)

BEIJING - Rais wa Russia Vladimir Putin amewasili Beijing jana Jumanne usiku kwa ziara ya kiserikali nchini China kutokana na mwaliko wa Rais wa China Xi Jinping, ziara yake hiyo nchini China imeanzia tarehe 19 hadi 20 Mei , na hiyo ni ziara yake ya 25 nchini China.

Wizara ya mambo ya nje ya China imesema, marais hao wawili watabadilishana maoni juu ya uhusiano wa pande mbili, ushirikiano katika sekta mbalimbali, na masuala ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa kwa pamoja.

Mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Russia na maadhimisho ya miaka 25 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Ujirani Mwema, Urafiki na Ushirikiano kati ya China na Russia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema pande hizo mbili zitachukua fursa hiyo kuendelea kuzidisha na kuinua uhusiano kati ya China na Russia, ili kuingiza utulivu na juhudi zaidi duniani.

Rais wa Russia Vladimir Putin akiwasili Beijing Mei 19, 2026, kwa ziara ya kiserikali nchini China. (Xinhua/Gao Jie)

Rais wa Russia Vladimir Putin akiwasili Beijing Mei 19, 2026, kwa ziara ya kiserikali nchini China. (Xinhua/Gao Jie)

Rais wa Russia Vladimir Putin akiwasili Beijing Mei 19, 2026, kwa ziara ya kiserikali nchini China. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa Russia Vladimir Putin akiwasili Beijing Mei 19, 2026, kwa ziara ya kiserikali nchini China. (Xinhua/Shen Hong)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha