Lugha Nyingine
Xi Jinping afanya mazungumzo na Vladimir Putin mjini Beijing

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mei 20, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo na Rais wa Russia Vladimir Putin ambaye alikuwa ziarani nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing jana Jumatano, ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kuongeza muda zaidi wa Mkataba wa Ujirani Mwema, Urafiki na Ushirikiano kati ya China na Russia.
Rais Xi amesema kuwa mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Russia na maadhimisho ya miaka 25 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Ujirani Mwema, Urafiki na Ushirikianokati ya China na Russia.
"Uhusiano kati ya China na Russia umefikia kiwango cha juu hatua kwa hatua hasa kwa sababu nchi hizi mbili zimeshikilia bila kulegalega kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa na uratibu wa kimkakati, zimepanua ushirikiano kwa pande zote, na pia zikiwa na dhamirio ya kithabiti zinalinda haki na usawa wa kimataifa na kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja," amesema.
Amesema zikiwa ni nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi kubwa muhimu duniani, China na Russia zinapaswa kufuata mtazamo wa kimkakati na kutupia macho siku za baadaye za muda mrefu, kusukuma mbele maendeleo na ustawishaji wa nchi kwa kupitia uratibu wa kimkakati wa sifa bora zaidi kwa pande hizo mbili, na kufanya juhudi za kuufanya mfumo wa usimamizi wa dunia kuwa wa haki na usawa zaidi.
Amesisitiza kwamba uhusiano kati ya China na Russia umeingia katika kipindi kipya cha kutimiza lengo la kupata mafanikio makubwa zadi na maendeleo ya haraka zaidi.
Pia amesisitiza juhudi za pamoja za kulinda kithabiti utaratibu wa kimataifa wa baada ya Vita vya Pili vya Dunia, na heshima na mamlaka ya sheria za kimataifa, kuwa na mshikamano na Nchi za Dunia ya Kusini, na kuelekeza mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa Dunia yaendelee kwa mwelekeo sahihi.
Kwa upande wake Rais Putin amesema uhusiano kati ya Russia na China, chini ya juhudi za pamoja za pande zote mbili, umefikia kiwango cha juu ambacho hakijawahi kufikia, ambapo mawasiliano kwenye ngazi ya juu yamekuwa karibu, na hali ya kuaminiana kisiasa imeendelea ipasavyo.
"Biashara za pande hizi mbili zinaongezeka kwa hatua madhubuti, utoaji na mahitaji ya nishati vinaendelea kwa kunufaishana, ushirikiano katika usafirishaji na uchukuzi, usambazaji bidhaa, sayansi na teknolojia unaendelea kwa kina siku hadi siku, na mawasiliano kati ya watu wa nchi hizi mbili yameonesha hali nzuri na mwelekeo mzuri," Putin ameongeza
Putin akisisitiza kwamba Mkataba wa Ujirani Mwema, Urafiki na Ushirikiano una umuhimu zaidi kwa hali ya hivi sasa, Russia inapenda kushirikiana na China katika kuendeleza mambo kwa kufuata moyo wa Mkataba huo, kuimarisha uratibu wa kimkakati na ushirikiano wa kufuata hali halisi, na kuhimiza uhusiano wa pande mbili hadi ngazi ya juu zaidi.
Marais hao pia wamebadilishana maoni juu ya hali ya Mashariki ya Kati na masuala mengine makubwa ya kimataifa na kikanda.
Pia wameshuhudia kusainiwa kwa nyaraka 20 za ushirikiano katika sekta za uchumi na biashara, elimu, na sayansi na teknolojia.
Katika ziara hiyo ya Rais Putin, China na Russia zimetoa taarifa ya pamoja, zikitetea dunia ya ncha nyingi na uhusiano wa kimataifa wa aina mpya.
Kabla ya mazungumzo yao, Rais Xi aliandaa hafla ya kumkaribisha Rais Putin nje ya Jumba la Mikutano ya Umma katikati mwa Beijing, hafla hiyo ikihusisha maonyesho ya bendi ya jeshi, kupewa heshima za salamu kwa mizinga 21, na kukagua gwaride.
Jumatano jioni, Rais Xi alifanya dhifa ya kumkaribisha mwenzake Putin kwenye Ukumbi wa Dhahabu wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mei 20, 2026. (Xinhua/Wang Ye)

Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Russia Vladimir Putin wakisaini taarifa ya pamoja kuhusu kuongeza zaidi uratibu wa kimkakati kwa pande zote na kuzidisha ujirani mwema, urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili baada ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Mei 20, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye alikuwa ziarani nchini China, katika uwanja ulio nje ya lango la mashariki la Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Mei 20, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye alikuwa ziarani nchini China, katika uwanja ulio nje ya lango la mashariki la Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Mei 20, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye alikuwa ziarani nchini China, katika uwanja ulio nje ya lango la mashariki la Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Mei 20, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye alikuwa ziarani nchini China, katika uwanja ulio nje ya lango la mashariki la Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Mei 20, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



