Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping na rais Putin wakishiriki kwenye hafla ya kufunguliwa kwa Mwaka wa Elimu wa China na Russia

Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Russia Vladimir Putin wakishiriki kwenye hafla ya kufunguliwa kwa Mwaka wa Elimu wa China na Russia kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mei 20, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Russia aliyekuwa ziarani nchini China Vladimir Putin walishiriki kwenye hafla ya kufunguliwa kwa Mwaka wa Elimu wa China na Russia kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing jana Jumatano.
Akihutubia hafla hiyo, Rais Xi amesema kwamba ushirikiano wa kielimu kati ya China na Russia umeendelezwa kwa kina na kupata mafanikio dhahiri katika miaka mingi iliyopita, na pia kuongeza maana ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa China na Russia katika zama mpya.
“Kwa kuchukua Mwaka wa Elimu wa China na Russia kuwa fursa, pande hizi mbili zinapaswa kupata maoni ya pamoja zaidi juu ya ushirikiano, kupanua maeneo ya ushirikiano na kuinua kiwango cha ushirikiano," Rais Xi amesema.
Ametoa wito wa kuzidisha ushirikiano katika kuwaandaa vipaji wa hali ya juu ili kukabiliana kwa pamoja na changamoto katika sayansi ya mambo mapya, na kusaidia maendeleo ya nchi hizo mbili ya kutegemea uvumbuzi.
Pia amesisitiza kufuata wazo la kufundishana kati ya ustaarabu, kuhimiza hali ya kurithisha ustaarabu na kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa elimu, na kuendeleza urafiki wa jadi ili kufungua zaidi nguvu bora za ushirikiano wa kielimu, na kuhimiza maelewano na urafiki miongoni mwa watu wa nchi hizo mbili.
Putin, ambaye alikuwa katika ziara ya kiserikali nchini China, amesema kufunguliwa kwa Mwaka wa Elimu wa Russia na China ni wenye umuhimu sana.
Amesema, kupitia kuimarisha ushirikiano wa kielimu, Russia inapenda kushirikiana na China katika kuongeza maelewano kati ya vijana wa nchi hizo mbili, kuhakikisha mambo ya urafiki kati ya Russia na China yanaendelezwa kizazi hadi kizazi, na kuhimiza maendeleo zaidi ya uhusiano wa pande mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



