Rais wa Cuba asema mashtaka ya Marekani dhidi ya Raul Castro ni “hila ya kisiasa” isiyo na msingi wa kisheria

(CRI Online) Mei 21, 2026

Rais Miguel Diaz-Canel wa Cuba amesema mashtaka ya serikali ya Marekani dhidi ya kiongozi wa Mapinduzi ya Cuba Raul Castro ni “hila ya kisiasa” isiyo na msingi wowote wa kisheria.

Diaz-Canel amesema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X jana Jumatano kwamba mashtaka hayo “yanaonyesha tu kiburi na mfadhaiko ambao wawakilishi wa kibeberu wanahisi mbele ya azma isiyoyumba ya Mapinduzi ya Cuba na umoja na nguvu ya kimaadili ya uongozi wake.”

Mapema siku hiyo ya Jumatano, jopo la majaji kutoka mahakama ya Wilaya ya Florida ya Marekani lilimshtaki Raul Castro kwa tuhuma za kutoa amri ya kutungua ndege mbili zilizokuwa zikiendeshwa na kundi la Wacuba waliopo uhamishoni nchini Marekani liitwalo “Brothers to the Rescue” mwaka 1996.

“Hii ni hila ya kisiasa, isiyo na msingi wowote wa kisheria, inayolenga tu kurundika faili za kughushi wanazotumia ili kuhalalisha uvamizi wao wa kijinga wa kijeshi dhidi ya Cuba.” Diaz-Canel ameandika akirejelea mashtaka hayo.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha