Ofisa mwandamizi wa CPC afanya ziara nchini Misri na Tanzania

(CRI Online) Mei 22, 2026

Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Bw. Liu Haixing ameongoza ujumbe wa CPC kufanya ziara nchini Misri na Tanzania kuanzia tarehe 17 hadi 20 Mei.

Kwenye ziara hiyo, kwa nyakati tofauti Liu alikutana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi cha Tanzania ambaye pia ni Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Spika wa Baraza la Juu la Bunge la Misri Essam El Din Farid, na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Ahmed Aboul Gheit.

Pia alishiriki kwenye mazungumzo kati ya vyama vya kisiasa vya China na Misri, na mazungumzo kati ya CPC na vyama sita vya ukombozi vya kusini mwa Afrika.

Aidha, Bw. Liu alihudhuria kwenye hafla za uzinduzi wa Kitengo cha Stadi za Fikra ya Kidiplomasia ya Xi Jinping katika Kituo cha Stadi na Utafiti cha Tahriri cha Misri, vilevile katika Kituo cha Utafiti cha Misri kuhusu Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China katika Zama Mpya kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Tanzania.

Katika ziara yake hiyo, Bw. Liu amefafanua fikra hiyo ya Xi Jinping, na kubadilishana mawazo na pande husika juu ya masuala makuu ya kimataifa na kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha