Trump asema yeye atakuwa mtu wa kuingilia kati ya mambo ya Cuba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 22, 2026

Rais wa Marekani Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari, South Lawn, Ikulu ya White House, Washington, D.C., Marekani, Mei 1, 2026. (Picha na Li Yuanqing/Xinhua)

Rais wa Marekani Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari, South Lawn, Ikulu ya White House, Washington, D.C., Marekani, Mei 1, 2026. (Picha na Li Yuanqing/Xinhua)

WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump amesema katika miongo kadhaa iliyopita, watangulizi wake kila mara walikuwa wakifikiria kuingilia kati mambo ya Cuba, na hali ya sasa inaonekana kuwa ni yeye ndiye atakayefanya hivyo.

"Marais wengine waliopita walikuwa wakifikiria kufanya jambo hili katika miaka 50, na 60 iliyopita," Trump amewaambia waandishi wa habari jana Alhamisi katika Ikulu ya White House. "Na, sasa inaonekana kuwa mimi ndiye mtu wa kufanya hivyo. Kwa hiyo, nitafurahia kufanya hivyo."

“Wamarekani wenye asili ya Cuba wanaweza kurudi Cuba na kusaidia,” ameongeza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema mapema siku hiyo ya Alhamisi kwamba uwezekano wa kufanya mazungumzo na kufikia makubaliano na Cuba si mkubwa kwa sasa.

Hivi karibuni Marekani imemshtaki kiongozi wa Mapinduzi ya Cuba Raul Castro kuhusika na tukio lililosababisha vifo la Jeshi la Cuba kudungua ndege mbili miaka 30 iliyopita, na kupeleka Kundi la Manowari za Nimitz za Kubeba Ndege za Kushambulia kwenda Karibiani, hatua hizo zimechukuliwa kuwa sehemu moja ya kampeni pana ya shinikizo dhidi ya Cuba.

Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel alisema juzi Jumatano kwamba mashtaka hayo ya Marekani dhidi ya Castro ni "mbinu ya kisiasa" isiyo na msingi wa kisheria, akiongeza kwamba Washington "inadanganya na kupotosha matukio yanayohusika na tukio hilo ya kudunguliwa kwa ndege ndogo za shirika la kigaidi la Brothers to the Rescue."

Alionya Jumatatu wiki hii kwamba shambulio lolote la kijeshi la Marekani dhidi ya Cuba litasababisha "umwagaji damu wenye matokeo yasiyohesabika" na athari mbaya kabisa kwa amani na utulivu katika Latini Amerika na Karibiani.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha