Wanaanga wa Shenzhou-23 waingia katika kituo cha anga ya juu cha China cha Tiangong

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 25, 2026

Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Safari ya Anga ya Juu cha Beijing Mei 25, 2026 ikionyesha wanaanga wa vyombo vya anga ya juu vya Shenzhou-21 na Shenzhou-23 wanapiga picha pamoja . (Xinhua/Jin Liwang)

BEIJING - Wanaanga watatu waliosafiri kwenye chombo cha anga ya juu cha China cha Shenzhou-23 wameingia katika kituo cha anga ya juu cha China cha Tiangong na kukutana na wanaanga wengine watatu leo Jumatatu, wakianza raundi mpya ya makabidhiano ya wanaanga ndani ya obiti.

Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limesema kuwa wanaanga hao wa Shenzhou-21 waliokuwa ndani ya Tiangong walifungua mlango majira ya saa 11:13 alfajiri (Saa za Beijing) na kuwakaribisha wanaanga hao wapya waliowasili.

Wanaanga wa vikundi hivyo viwili walipiga picha pamoja kwa kumbukumbu za kukutana kwa mara ya nane kwenye anga ya juu katika historia ya usafiri wa vyombo vya China kwenye anga ya juu.

CMSA imesema wanaanga hao watafanya kazi ya makabidhiano ndani ya kituo hicho cha anga ya juu.

Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Safari ya Anga ya Juu cha Beijing Mei 25, 2026 ikionyesha wanaanga wa vyombo vya anga ya juu vya Shenzhou-21 na Shenzhou-23 wakizungumza kwenye chombo cha usafiri wa anga ya juu. (Xinhua/Jin Liwang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha