Lugha Nyingine
Xi atoa mwito wa kujenga haraka zaidi jumuiya ya China na Pakistan yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mei 25, 2026. (Xinhua/Li Xiang)
BEIJING - China na Pakistan zinapaswa kuharakisha ujenzi wa jumuiya ya China na Pakistan yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, na kupata matokeo zaidi katika ushirikiano wa hali zote kati ya nchi hizo mbili, Rais wa China Xi Jinping amesema Jumatatu alipokutana na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif mjini Beijing.
Pia amezihimiza pande hizo mbili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi zote mbili, kuchangia katika kuhimiza amani na utulivu wa kikanda, na kuweka mfano wa kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja na nchi jirani.
"Tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 75 iliyopita, China na Pakistan zimeunda urafiki wa jadi usiovunjika," Xi amesema, akieleza kuwa kuaminiana kimkakati na kufanya ushirikiano wa kufuata hali halisi kati ya pande hizo mbili kumehimiza kwa ufanisi maendeleo ya kila nchi.
Amesema China wakati wote inatoa kipaumbele cha juu kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Pakistan katika mambo ya diplomasia yake ya ujirani bila kujali namna hali ya kimataifa inavyobadilika.
"Pande zote mbili zinapaswa kufanya ushirikiano wa kiusalama kwenye kiwango cha juu zaidi na katika nyanja pana zaidi ili kudumisha kwa pamoja amani na utulivu wa kikanda," Xi amesema, akiongeza kuwa China inaipongeza Pakistan kwa kufanya kazi ya kusuluhisha katika kuhimiza kurejesha amani ya Mashariki ya Kati.
"Pande zote mbili zinapaswa kuendelea kudumisha mawasiliano na uratibu wa karibu, kupinga kwa pamoja hatua za upande mmoja na mawazo ya Vita Baridi, na kushirikiana pamoja katika kuhimiza dunia yenye ncha nyingi iliyo ya usawa na utaratibu na utandawazi wa uchumi duniani ulio wa jumuishi kwa wote," Xi ameongeza.
Sharif amesema Rais Xi ni rafiki mkubwa wa watu wa Pakistan, na pia rafiki mkubwa wa watu wote wapenda amani duniani.
"Chini ya uongozi imara wa Rais Xi, uchumi wa China umepata mafanikio makubwa yanayovutia ufuatiliaji duniani, na kutoa uhakikisho thabiti kwa ajili ya kulinda amani ya dunia na kujenga dunia ya ncha nyingi," Sharif amesema.
Amesema Pakistan inafuata kwa uthabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, inaunga mkono kithabiti msimamo wa China kuhusu masuala yote yanayohusiana na maslahi yake ya kimsingi, na daima itakuwa rafiki na mshirika mzuri wa China.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mei 25, 2026. (Xinhua/Shen Hong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



