Kundi la Mabalozi wa Afrika nchini China waandaa Mapokezi ya Siku ya Afrika Kuadhimisha Miaka 63 ya AU

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 26, 2026

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Miao Deyu akihudhuria na kutoa hotuba kwenye hafla iliyoandaliwa na Kundi la Mabalozi wa Afrika nchini China kusherehekea "Siku ya Afrika" mjini Beijing, Mei 25, 2026. (CMFA/People’s Daily Online)

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Miao Deyu akihudhuria na kutoa hotuba kwenye hafla iliyoandaliwa na Kundi la Mabalozi wa Afrika nchini China kusherehekea "Siku ya Afrika" mjini Beijing, Mei 25, 2026. (CMFA/People’s Daily Online)

Kundi la Mabalozi wa Afrika nchini China (GAAC) limeandaa hafla ya mapokezi ya kidiplomasia ya ngazi ya juu jana Jumatatu jioni mjini Beijing kuadhimisha Siku ya Afrika 2026, ikiwakutanisha Wakuu wa Balozi na wanadiplomasia wa Afrika, mabalozi kutoka makundi mengine ya kikanda, maofisa waandamizi wa Serikali ya China, mawaziri wa Afrika walioko ziarani China, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, wajumbe wa diaspora wa Afrika, viongozi wa kibiashara, wasomi, na marafiki wa muda mrefu wa Afrika nchini China.

Maadhimisho hayo ya mwaka huu yameelezwa kubeba umuhimu wa kipekee wa kihistoria kwani yanaashiria kumbukumbu ya miaka 63 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (OAU), ambayo sasa ni Umoja wa Afrika (AU), iliyoanzishwa Mei 25, 1963, vilevile kumbukumbu ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi za Afrika na Jamhuri ya Watu wa China.

Hafla hiyo ilipata heshima ya uwepo wa watu kadhaa mashuhuri, wakiwemo Carmen Ivelize Van-Dúnem do Sacramento Neto dos Santos, Waziri wa Uvuvi na Rasilimali za Baharini wa Jamhuri ya Angola; Alexander Nuetah, Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Liberia; na Francess Paige Alghali, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Sierra Leone.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Miao Deyu, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, ambaye uhudhuriaji wake umeelezwa kuonyesha umuhimu mkubwa unaowekwa na Serikali ya China kwa uhusiano kati ya Afrika na China na kuendelea kuimarisha kwa kina ushirikiano wa kimkakati kati ya Afrika na China.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika chini ya kaulimbiu ya Umoja wa Afrika ya 2026, "Kuhakikisha Upatikanaji Endelevu wa Maji na Mifumo Salama ya Usafi wa Mazingira ili Kufikia Malengo ya Ajenda ya 2063," yamesisitiza umuhimu wa maendeleo endelevu, usimamizi wa mazingira, usalama wa chakula, afya ya umma, na ushirikiano wa kikanda katika kusukuma mbele vipaumbele vya maendeleo vya muda mrefu vya Afrika. Aidha, Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, ambaye pia Mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika alitoa hotuba iliyorekodiwa kwa njia ya video ukumbini.

Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, ambaye pia ni Mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika. (People’s Daily Online)

Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, ambaye pia ni Mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika. (People’s Daily Online)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha