Waziri wa Mambo ya Nje wa China asisitiza mchango uliotolewa na China kwa mambo ya Umoja wa Mataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akiongoza mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama kuhusu kushikilia nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa na kuimarisha mifumo ya kimataifa ambayo Umoja wa Mataifa ni kiini, mkutano huo ulifanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Mei 26, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

UMOJA WA MATAIFA - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi jana Jumanne katika mkutano wa wazi wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama kuhusu kushikilia nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa na kuimarisha mifumo ya kimataifa ambayo Umoja wa Mataifa ni kiini, ambapo ametoa ripoti juu ya mchango uliotolewa na China kwa mambo ya Umoja wa Mataifa.

"Mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 55 tangu kurejeshwa kwa kiti halali cha Jamhuri ya Watu wa China katika Umoja wa Mataifa. Katika miaka 55 iliyopita, China ikiwa mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama, imeshiriki kwa juhudi zaidi katika mambo ya Umoja wa Mataifa," amesema Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Amesema chini ya hali ya kimataifa yenye msukosuko na mabadiliko, China inanyanyua bendera yake juu. Amesema matarajio muhimu ya China ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na mapendekezo manne makubwa kuhusu dunia vimepata uungaji mkono mkubwa duniani.

"Katika hali ambayo migogoro inatokea mara kwa mara duniani, China inahimiza amani na inahamasisha mazungumzo. China inafuata njia yake ya kipekee ya kutatua matatizo ya migogoro, ikiwa ni pamoja na kuanzisha Kundi la Nchi Marafiki kwa Amani juu ya mgogoro wa Ukraine kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa, ikichangia hekima na juhudi za China kila mara kwa ajili ya kudumisha amani ya dunia," amesema Wang.

Amesema Pendekezo la Maendeleo ya Dunia limekusanya mitaji ya dola za Marekani zaidi ya bilioni 23, mitaji hiyo imeunga mkono miradi zaidi ya 1,800 ya ushirikiano, kutoa miradi karibu 10,000 ya ujenzi wa uwezo kwa nchi zinazoendelea, na kutoa mafunzo kwa wataalamu zaidi ya 200,000 katika sekta mbalimbali. "Hayo yote yametoa msukumo mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya Nchi za Kusini ya Dunia," ameongeza.

Wang amesema katika wakati wa kutokea kwa misukosuko mikubwa ya umma, China inakimbilia kutoa msaada. Mwaka 2015, China ilitoa uungaji mkono kwa nguvu zote kwa nchi tatu za Afrika Magharibi katika kupambana na virusi vya Ebola. Amesema China inapenda kuzisaidia kwa iwezekanavyo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda katika kukabiliana na mlipuko wa sasa wa Ebola,. "Tunapozungumza sasa, timu za madaktari wa China ziko katika kushirikiana bega kwa bega na ndugu za Afrika kwenye mstari wa mbele wa kupambana na ugonjwa huo.

"Katika wakati wa kukabiliwa na changamoto dhidi ya ushirikiano wa pande nyingi, China inasimama kubeba wajibu," amesema Wang, akitaja China ni nchi mchangiaji mkubwa wa pili katika bajeti ya kawaida ya Umoja wa Mataifa, imeweka na kutumia vizuri Mfuko wa Amani na Maendeleo wa China na UN na Mfuko wa Maendeleo ya Dunia na Ushirikiano wa Kusini na Kusini, na kupendekeza kuanzishwa kwa Shirika la Kimataifa la Upatanishi na Shirika la Data Duniani n.k.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akiongoza mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama kuhusu kushikilia nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa na kuimarisha mifumo ya kimataifa ambayo Umoja wa Mataifa ni kiini kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Mei 26, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha