Lugha Nyingine
Jukwaa la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari la China-Kyrgyzstan 2026 lafanyika Bishkek

Jukwaa la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari la China-Kyrgyzstan 2026 likifanyika Bishkek, Kyrgyzstan Mei 27, 2026, chini ya kaulimbiu ya "Kuzidisha ushirikiano wa vyombo vya habari vya China-Kyrgyzstan kwa mustakabali mzuri zaidi wa SCO." (Picha na Xue Ke/Global Times)
Jukwaa la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari la China-Kyrgyzstan 2026 limefanyika Jumatano huko Bishkek, Kyrgyzstan, chini ya kaulimbiu ya "Kuzidisha Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Kyrgyzstan kwa Mustakabali Mzuri zaidi wa SCO," ambapo washiriki karibu 100, wakiwemo wawakilishi wa vyombo vya habari, maafisa wa serikali, wataalam, wasomi na viongozi wa wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili walihudhuria jukwaa hilo na kushiriki katika mabadilishano na mijadala ya kina kuhusu mada za maendeleo ya uchumi na biashara, mabadilishano ya kitamaduni, na ushirikiano wa vyombo vya habari.
Washiriki wamebainisha kuwa uhusiano kati ya China na Kyrgyzstan umeendelea kuongezeka na kuzidishwa katika zama mpya. Wamesisitiza kwamba vyombo vya habari vya nchi zote mbili vinapaswa kubeba majukumu yao, kujenga maafikiano juu ya maadili ya pamoja, kuakisi matarajio ya watu wa nchi zote mbili ya kutaka maisha bora, na kwa pamoja kusimulia simulizi za ujirani mwema, urafiki na ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Kyrgyzstan.
Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO). Washiriki wa jukwaa hilo wanaamini kwamba kwa kushikilia Moyo wa Shanghai wa kuaminiana, kunufaishana, usawa, mashauriano, kuheshimu tofauti za ustaarabu na kutafuta maendeleo ya pamoja, jumuiya hiyo imedumisha kasi imara ya ukuaji.
Wanaamini kwamba vyombo vya habari vya nchi wanachama wa SCO vinapaswa kutumia kikamilifu majukumu yao ya kuwa madaraja na viungo, kuhimiza Moyo wa Shanghai, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo, na kuongeza uhusiano wa kati ya watu, hivyo kuchangia hekima na nguvu katika kujenga maskani nzuri zaidi ya SCO.
Cui Shixin, Naibu Mhariri Mkuu wa Gazeti la People's Daily, katika hotuba yake ya ufunguzi amesema kuwa Mkutano ujao wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa SCO utafanyika Bishkek katika nusu ya pili ya mwaka 2026. Amesema zikiwa zimeunganishwa na milima na mito, China na Kyrgyzstan ni majirani wema, marafiki makubwa na washirika wazuri wenye uhusiano wa karibu wa watu. Amesema, katika wakati huu muhimu, kufanya Jukwaa la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari la China-Kyrgyzstan ili kutafuta namna ya kubeba majukumu na dhamira za vyombo vya habari vya nchi hizo mbili katika zama mpya ni katika muda muafaka na kwenye umuhimu mkubwa. Amesema hatua hiyo si tu inaweka katika vitendo makubaliano muhimu yaliyofikiwa na Rais Xi Jinping na Rais Sadyr Japarov kuhusu kuzidisha uhusiano wa washirika wa kimkakati wa pande zote kwa zama mpya, bali pia inamaanisha hatua imara ya kuunda mazingira mazuri ya maoni ya umma na kuimarisha msingi wa umma mpana kwa Mkutano huo ujao wa Bishkek wa SCO.
Salkyn Sarnogoeva, Naibu Waziri wa Utamaduni, Habari, Michezo na Sera ya Vijana wa Jamhuri ya Kyrgyzstan, katika hotuba yake amebainisha kuwa mafungamano ndani ya mfumo wa SCO hayahusu tu miradi ya uchumi na makubaliano ya kisiasa. Amesema, zaidi ya yote, yanawakilisha muunganiko wa tamaduni na simulizi za binadamu. Amesema, ni watendaji wa vyombo vya habari wanaotafsiri lugha tata ya diplomasia ya jadi katika simulizi za urafiki, ushirikiano na maendeleo ya kiujenzi yanayoeleweka kwa raia wote. Amebainisha kwamba, kwa sasa SCO iko katika awamu ya maendeleo makubwa, huku sekta ya vyombo vya habari ikiwa na nafasi muhimu ya kimkakati.
Jukwaa hilo limeandaliwa kwa ushirikiano na People's Daily na Kyrgyz Tuusu Publishing House. Shughuli hiyo ilijumuisha hotuba kuu na mijadala ya wanajopo ya kujadiliana kwa zamu, pamoja na "Maonyesho ya Picha ya 'Kuunganishwa na Milima na Mito, Kufungamanishwa kwa Mioyo ya Pamoja - China na Kyrgyzstan Bega kwa Bega kwa Mustakabali wa Siku za Baadaye'" na shughuli ya 'Wiki ya China Nje ya Nchi' ya kituo cha Global Times tawi la Kyrgyzstan.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



