Lugha Nyingine
DRC yasema mlipuko wa Ebola bado uko katika kipindi cha mwanzo lakini idadi ya wagonjwa inaongezeka

Wafanyakazi wa matibabu wakivaa suti za kujikinga kabla ya kazi ya kunyunyuzia dawa kuua vijidudu maradhi, huko Mongbwalu, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mei 24, 2026. (Xinhua)
KINSHASA - Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Roger Kamba amesema Mlipuko wa Ebola nchini humo bado uko katika kipindi cha mwanzo, lakini maambukizi na vifo vinaendelea kuongezeka.
Mamlaka za afya zimewagundua wagonjwa wanaoshukiwa takriban 1,000 katika maeneo yaliyoathiriwa, ambapo 101 wamepimwa na kukutwa na virusi, Kamba ameuambia mkutano na waandishi wa habari Jumanne wiki hii.
Amesema takwimu zilizotolewa kwa hatua ya kwanza zinaonyesha kwamba vifo takriban 200 hadi 220 vinaaminika kuhusika na mlipuko huo, na vifo 17 vimethibitishwa kupitia vipimo vya kwenye maabara.
"Bado tuko mwanzoni mwa janga," Kamba amesema, akiongeza kuwa muda wa hivi sasa unaoendelea kuongezwa kwa wgonjwa utategemea ufanisi wa juhudi za kukabiliana na ugonjwa. Waziri huyo amesema mamlaka zinapanga operesheni ya kukabiliana na ugonjwa huo inakadiriwa kuendelea kwa miezi minne hadi sita.
Mlipuko huo umesababishwa na virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo, ambayo Kamba ameielezea kuwa si hatari sana kuliko aina ya Zaire lakini bado ni hatari kama idadi ya watu walioambukizwa itaendelea kuongezeka. Kwa sasa hakuna chanjo iliyoidhinishwa au matibabu maalum juu ya Ebola ya Bundibugyo.
Amesema ili kudhibiti maambukizi, mamlaka zinategemea ufuatiliaji, upimaji, kutenganisha watu, kufuatilia watu waliogusana au kukutana na watu walioambukizwa, maeneo ya wakazi kushiriki kwenye kazi husika na kufanya mazishi salama.
Siku ya Jumamosi, serikali ilisimamisha usafiri wa ndege za abiria kwenda na kutoka Bunia, mji mkuu wa Jimbo la Ituri na ambao ni eneo lililoathirika zaidi na mlipuko huo, lakini ndege za kutoa huduma za kibinadamu bado zinaendelea kutoa huduma.
Kamba amesema virusi hivyo huenda vilikuwa vikisambaa kabla ya mlipuko huo kutangazwa rasmi Mei 15, na akitaja muda mrefu wa kipindi cha kuzaliana na kukua kwa virusi vya Ebola unaweza kufikia siku 21. Ameongeza kuwa mamlaka za afya bado hazijatambua "mgonjwa wa mwanzo kabisa" wa mlipuko huo wa sasa.

Wakazi waliovaa barakoa wakionekana Mongbwalu, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mei 24, 2026. (Xinhua)

Wafanyakazi wa matibabu wakivaa suti za kujikinga kabla ya kazi ya kunyunyuzia dawa kuua vijidudu maradhi, huko Mongbwalu, Jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mei 24, 2026. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



