Mitazamo mitatu ya Upunguzaji Umaskini Nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2026

Watalii wakichuma matunda ya cheri kwenye bustani katika mtaa wa Guojia mjini Leling, China Mei 28. (Picha na Jia Peng/Visual People)

Watalii wakichuma matunda ya cheri kwenye bustani katika mtaa wa Guojia mjini Leling, China Mei 28. (Picha na Jia Peng/Visual People)

Umaskini ni tatizo lililodumu kwa muda mrefu la jamii ya binadamu, na kuutokomeza ni lengo la pamoja miongoni mwa nchi duniani kote.

Tarehe 27 Mei, Jukwaa la Ngazi ya Juu kuhusu Kupunguza Umaskini na Kupata Maendeleo 2026 lilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Beijing, China. Mwaka huu, kaulimbiu ya jukwaa hilo ni "Kuunganisha Nguvu Duniani ili Kuhimiza Upunguzaji Umaskini." Wawakilishi kutoka nchi na maeneo zaidi ya 40 – pamoja na maafisa kutoka mashirika ya kimataifa na wasomi mashuhuri walikusanyika Beijing kushiriki katika mijadala inayohusu kaulimbiu hiyo. Hasa, jitihada za China katika kupunguza umaskini ziliibuka kuwa jambo kuu la kufuatiliwa kwa washiriki wote.

Mtazamo wa Kwanza: Takwimu

Katika jukwaa hilo, maonyesho yaliyopewa kichwa cha "Kuondoa Umaskini uliokithiri: Kusukuma Mbele Ustawishaji wa pande zote wa Vijijini" yalivutia wageni wengi, ambao waliangalia vitu vilivyokuwa vikioneshwa na kujadiliana. Takwimu zilizokuwa zikioneshwa kwenye mabango zinasimulia maendeleo na mabadiliko makubwa ya maeneo ya vijijini ya China, wakati huohuo zikichora picha ya kugusa moyo ya jitihada za China za kupunguza umaskini.

Kutoka watu milioni 98.99 kwenda chini hadi 0, hiyo inawakilisha mabadiliko katika idadi ya watu maskini wa vijijini nchini China tangu kuzinduliwa kwa kampeni ya nchi nzima dhidi ya umaskini. Baada ya miaka 8 ya juhudi mfululizo, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2020, watu wote milioni 98.99 wa vijijini waliokuwa wakiishi chini ya mstari wa umaskini uliowekwa wakati huo walikuwa wameondolewa kutoka kwenye umaskini, na aidha, wilaya zote 832 zilizokuwa maskini zimeondolewa katika orodha ya wilaya maskini, na vijiji vyote 128,000 vilivyokuwa maskini vimeondolewa katika orodha hiyo vilevile.

China imeshinda mapambano dhidi ya umaskini, ikifikia malengo ya kupunguza umaskini yaliyowekwa katika Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa 2030 miaka 10 kamili kabla ya muda uliopangwa. "Mafanikio ya China katika kupunguza umaskini ni ya kustaajabisha. Mafanikio ya namna hiyo ni ya China bali pia yana mchango mkubwa kwenye mapambano ya kutokomeza umaskini duniani, na yameweka mfano wa kuigwa kwa dunia nzima." Stephen Jackson, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini China, amesema katika jukwaa hilo.

Mtazamo wa Pili: Swali Moja

Kuhusu kusukuma mbele upunguzaji wa umaskini, kama China imefanikiwa, je, inawezekana nchi zingine zinazoendelea pia kufanikiwa? Katika jukwaa hilo, wageni washiriki walijikita katika swali hili hasa, na kujadili kwa kina umuhimu kwa dunia wa jitihada hizo za China za kupunguza umaskini.

Katika mjadala wa jukwaa tanzu, Profesa Li Xiaoyun, Mwalimu wa Sayansi za Jamii katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, alitoa mifano miwili. Wa kwanza unahusu mahindi: miaka zaidi ya 10 iliyopita, Li Xiaoyun na timu yake walianzisha teknolojia ya China ya kupanda mahindi kwa msongamano katika vijiji vya Mkoa wa Morogoro, Tanzania. Wakifanya shughuli zao chini ya hali ya mtaji mdogo, walitumia kikamilifu uwezo bora wa maeneo husika wa uwepo wa nguvukazi nyingi ili kuongeza mazao kwa kupunguza umbali kati ya mistari, kuongeza idadi ya mimea na kutumia mbinu makini za usimamizi. Mfano wa pili ni kuhusu maharage ya soya. Wakikabiliana na tatizo la maeneo husika la ukosefu wa vifaa vya usindikaji na umeme wa uhakika, timu hiyo ya Profesa Li Xiaoyun ilipeleka mashine ndogo za jadi za China za kusaga mawe katika maeneo hayo. Kwa kutumia zana hizo, waliandaa vyakula vya kifungua kinywa kwa kutumia maziwa ya soya na maganda ya maharage ya soya, na hivyo kuboresha kwa ufanisi lishe ya watoto wenyeji.

Wakiunganisha safari kutoka jitihada za China za kupunguza umaskini na maendeleo duniani, washiriki kwa ujumla walifikia maafikiano mapana: hatua na uzoefu wa China katika kupunguza umaskini vinaipa dunia utajiri wa "hekima ya China" na "masuluhisho ya China". Kama China imeweza kufanikiwa, nchi zingine zinazoendelea zinaweza pia kufanikiwa.

Mtazamo wa Tatu: Muungano Mmoja

"Katika kukabiliana na changamoto, tunaamini kithabiti kwamba ni kupitia tu kuwa na maafikiano ya kimataifa, kuhamasisha rasilimali za wadau mbalimbali, na kuzidisha ushirikiano wa washirika ndipo tunaweza kujenga vichocheo vipya kwa ajili ya kupunguza umaskini na kupata maendeleo, na kwa pamoja kuingia katika zama mpya ya kupunguza umaskini na kupata maendeleo."

Tarehe 27 Mei, katika Jukwaa hilo la Ngazi ya Juu la Kupunguza Umaskini na Kupata Maendeleo 2026, Muungano wa Marafiki wa Kupunguza Umaskini na Kupata Maendeleo ulitangazwa rasmi kuanzishwa. Sentensi iliyonukuliwa hapo juu imechukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye tamko la kuanzishwa kwa muungano huo.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, Muungano huo umeanzishwa kwa pamoja na China, nchi zingine 53 na mashirika 9 ya kimataifa. Unasisitiza waziwazi kuheshimu haki huria ya kila nchi ya kuchagua mikakati ya kupunguza umaskini na kupata maendeleo iliyo mwafaka kwa hali zake halisi za kitaifa, kuhimiza ubadilishanaji wa uzoefu wa kimataifa katika kupunguza umaskini, na kuchunguza kwa pamoja njia za kutokomeza umaskini kimsingi.

Kwa kutazama mustakabali wa siku za baadaye, na kama ilivyoelezwa kwenye tamko la kuanzishwa kwa muungano huo: Hebu tushikilie moyo wa mustakabali wa pamoja duniani na mshikamano wa kushirikiana ili kujenga kwa pamoja dunia bora, ambayo haina umaskini na yenye sifa ya ustawi wa pamoja!

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha