Lugha Nyingine
Xi Jinping ahimiza watoto kurithisha desturi za mapinduzi
BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa wito wa kurithisha desturi za mapinduzi katika barua ya majibu kwa wanafunzi waelezaji wa majumba ya makumbusho ya sehemu za kuzaliwa kwa CPC katika Mji wa Shanghai na Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China.
Rais Xi, amewahimiza kuongeza ujuzi na uwezo, na ametoa salamu za Siku ya Watoto Duniani kwa watoto kote nchini China.
Wanafunzi waelezaji hao hivi karibuni walimwandikia barua Rais Xi, wakimwelezea kile walichojifunza na kupata wakati walipokuwa wakifanya kazi ya kujitolea kuwa waelezaji katika jumba la makumbusho ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa CPC mjini Shanghai, na Jumba la Makumbusho ya Mapinduzi la Nanhu mjini Jiaxing, Zhejiang.
Katika barua hiyo iliyoandikwa Jumamosi, Rais Xi amesema amefurahi kujua kwamba wanafunzi hao wamejenga upendo wa kina kwa Chama, nchi, na ujamaa kwa kupitia kusimulia historia ya Chama, hadithi za mapinduzi, na vitendo vya mashujaa.
"Mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 105 tangu kuanzishwa kwa CPC. Mambo ya Chama yanahitaji juhudi zinazoendelea kufanywa na watu wa vizazi kadhaa ," Rais Xi amesisitiza, akihimiza wanafunzi hao kuendelea kukiunga mkono Chama, kujijengea sifa na mienendo yao, na kupokezana majukumu ya kihistoria katika safari mpya.
Mapema ya mwaka 2021, pendekezo moja lilianzishwa kote nchini la kuwatia moyo watoto wa shuleni kusoma historia ya Chama na kutoa simulizi husika kwenye majumba ya ukumbusho wa mapinduzi.
Mkutano Mkuu wa Kwanza wa CPC ulifanyika Shanghai mwezi Julai mwaka 1921. Kisha waanzilishi walihamia ndani ya mashua kwenye Ziwa Nanhu mjini Jiaxing ili kumaliza mkutano huo wa kihistoria, ambapo walipitisha mwongozo na azimio la kwanza la Chama. Mashua hiyo ya alama ya kihistoria sasa inajulikana kwa jina la Mashua Nyekundu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



