Timu ya madaktari ya China yaadhimisha Siku ya Watoto kwa huduma ya matibabu bila malipo nchini Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 02, 2026

Wajumbe wa kundi la 28 la timu ya madaktari ya China katika Tanzania Bara wakimwelekeza mwanafunzi mbinu za ufufuaji wa moyo na mapafu (CPR) shuleni jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 1, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Wajumbe wa kundi la 28 la timu ya madaktari ya China katika Tanzania Bara wakimwelekeza mwanafunzi mbinu za ufufuaji wa moyo na mapafu (CPR) shuleni jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 1, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM - Kundi la 28 la timu ya madaktari ya China katika Tanzania Bara limefanya shughuli ya huduma ya matibabu bila malipo jana Jumatatu katika shule jijini Dar es Salaam, likitoa mashauriano na elimu ya afya ya umma bila malipo kwa walimu na wanafunzi.

Liu Jia, mkuu wa timu hiyo ya madaktari, amesema shughuli hiyo, ambayo ni sehemu ya mpango wa "Timu 100 za Madaktari katika Vijiji 1,000" wa China, iliwaleta pamoja wataalamu kutoka taaluma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na upasuaji wa moyo, upasuaji wa neva, watoto, ganzi, mifupa na otolaryngoloji. Walimu na wanafunzi zaidi ya 300 walipokea huduma za matibabu kwenye shughuli hiyo.

Timu hiyo pia iliendesha vipindi vya mafunzo juu ya ufufuaji wa moyo na mapafu, mbinu za Heimlich, na kinga na udhibiti wa Ebola. Kampuni ya Uhandisi wa Reli ya Jianchang ya China ilijiunga na timu hiyo ya madaktari katika kuchangia vifaa vya shule na dawa zinazotumika mara kwa mara shuleni.

Jamaldini Hassan Mohamed, mkuu wa shule hiyo, amesema shughuli hiyo ya huduma ilikuwa zawadi maalum na yenye thamani kwa wanafunzi katika kusherehekea Siku ya Watoto Duniani.

"Timu ya madaktari ya China si tu imetoa huduma za matibabu kwa walimu na wanafunzi lakini pia imetoa maarifa juu ya huduma ya kwanza na uzuiaji magonjwa, ikiwasaidia watoto kujenga uelewa mkubwa zaidi wa afya," amesema.

Akitoa shukrani kwa uungaji mkono wa muda mrefu unaotolewa na timu ya madaktari ya China kwa huduma za elimu na afya za wenyeji, amesema anatumai shughuli kama hizo za mabadilishano zitaendelea katika siku zijazo.

Liu amesema kuwa urafiki kati ya China na Tanzania una historia ndefu na kwamba kulinda afya ya watoto wenyeji ni jukumu muhimu la timu hiyo ya madaktari ya China

"Timu ya madaktari wa China itaendelea kufanya mashauriano ya matibabu, elimu ya afya, na programu za usaidizi bila malipo, ikitumia huduma ya afya kama daraja la kuimarisha zaidi urafiki mkubwa kati ya watu wa China na Tanzania," ameongeza.

Wajumbe wa kundi la 28 la timu ya madaktari ya China katika Tanzania bara wakifanya uchunguzi wa sikio kwa mwanafunzi shuleni jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 1, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Wajumbe wa kundi la 28 la timu ya madaktari ya China katika Tanzania bara wakifanya uchunguzi wa sikio kwa mwanafunzi shuleni jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 1, 2026. (Xinhua/Emmanuel Herman)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha