Kijana wa Marekani ajionea jukwaa la mtindo la kijijini mkoani Guizhou

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 02, 2026

Jukwaa la maonyesho lenye mambo ya mitindo zaidi haliko Paris wala Milan, bali linapatikana kwenye Jukwaa la Kijiji katika mji wa Kaili, eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Wadong la Qiandongnan, Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China.

Tofauti na wiki za mitindo za kawaida, jukwaa hili la kijijini haliweki vizuizi kuhusu uanamitindo wa kitaalamu. Hapa, iwe wakulima, walimu, wanafunzi au watalii... kila watu wa kawaida kutoka makundi yote ya kijamii wanaweza kupanda jukwaani na kuchukua nafasi ya kuwa nyota wa kutazamwa na kufuatiliwa zaidi na hadhira.

Wakiwa wamevalia mavazi ya kipekee ambayo huchanganya mambo ya utamaduni wa makabila ya Wamiao na Wadong, hawaonyeshi tu uzuri wa mitindo, bali pia wanaonyesha upendo na kujiamini zaidi kwa utamaduni wa nyumbani. Fuatana na Michael kutoka People’s Daily Online akitembelea mji huo wa Kaili ili ujionee mwenyewe haiba hii ya kipekee! 

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha